Mtitu: Sababu ya kuamua kuzambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuuza Steps Entertainment

Mtitu: Sababu ya kuamua kuzambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuuza Steps Entertainment

Bongo movies akipewa kagali ka mtumba na dola 1000,basi anajiona michael jackson.na akipita kwa shigongo akauza story mbili tatu ta kujikuza basi tena anasahau kila kitu haya ndo matokeao yako,ni msaniii yupi wa BONGO STAR SEARCH ANA MAISHA YALIONYOOKA NA YANAYOELEWEKA LEO?TAFAKARI CHUKUA ATUA

haya ya maajabu makubwa. msanii anatakiwa kufaidika na kila nakala ya kazi yake. ni makosa makubwa kuuza jumla hakimiliki ya kazi yako. nakutakia mafanikio Ndugu Mtitu endelea kuonesha njia!
 
Hongera ndugu kwa kuanzaa safari mpya ambayo inaonesha kweli utafika kileleni.. ukaishi maisha mazuri kwa kazi zakoo za sanaa. Endelea kujisimamia mwenyewe ili uvune zaidi mapato. Wasanii wenzako wanao kuona wewe mnafki na msaliti kwa kuikimbia kambia ya STEPS ENT. achana nao wala wasikurudishe kwenye huo ukoloni mambo leo unao endelea kuwakabili na kuwatafuna.
Nime sikitika kuona mnauza haki zenu na sijui mtajivunia nini sasa siku za usoni.??
mmeyasikia yalio mkuta saida karoli yule dada wa mziki, tabia hizo hizo za kuuza kazi zenu leo meneja wake anaenda kujiingizia pesa kirahisi na kutajirika maradufu baada ya wimbo wa saida kutumika kwenye movie marekani na kwa maelezo ya meneja anajianda kudai alipwe kutokana na wimbo huo kutumika na kwa upande wa saida hana haki na wimbo huo kwa kua alisha uza album kwa meneja kwahiyo saida kupata kidogo kwa kile atakacho lipwa meneja ita tegemeana na mapenzi ya meneja mwenyewe. Maskini dada wa watu kachambua kama karanga mpaka marekani leo hii apati kitu..!!!!?
Bongo movie nako kumbe mambo hivyo hivyo, mnauza kazi zenu jumla mwisho wasiku mnabaki maskini.
Nawaonea huruma ingawa na nyie mnatuibia wananchi pesa zetu kwa kutu tolea movie mbovu mbovu, hamna uharisia,kazi hazina ubora. Basi uwizi tu.
 
Akili za bongo movie,kwanini sasa usijitaje jina kabisa wakati ushataja scenerio na cheo chako?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kumbe mnakwendaga ikulu kujadiliana na mkulu mambo ya bongo movie?
Very cheap president.
 
So touching. all the best aisee. natam
ani wasanii wote wangekuwa na ujasiri kama wako.
 
...ila mtitu nae anajua kutumia fursa,kwaya zinamfahamu uzuri...
 
Hii thread imenipa uamsho sana natamani hata nikawashike vichwa hawa wasanii jamani waelewe!!! Kwani mtu ukijisambazia filamu zako mwenyewe unapigwa na hao steps!?

Yaani m2 anakaa tu kwenye kiti anasubiri pesa iingie wakati msanii ameuza nyago vya kutosha wanishia kumeza kashfa tu na maisha ya kusota..yaani jamani jana nilisikitika sana nilikutana na msanii flani wa filamu jamani amechoka hadi huruma!! Wakati ndo alikuwa anajina kubwa tu enzi hizo.

Jamani wasanii muimarike kiakili na muanze kujituma
 
TEAMNYATI AND TEAMANACONDA NJO VILE HABARI YA MUJINI MUKUYE KWENYE HZO TEAM.

.......................................
Ukipata Ujumbe wa chuki au matusi futa delete kabisa.
.......................................
 
Nakunukuu:
"... ndani ya masaa matano ya
kwanza nilifanikiwa kurudisha gharama zangu
zote na kupata faida kidogo..." haaa Tanzania hii au wapi?
 
Mkuu Carter.....wacha nikueleze kitu ambacho watu wengi hawakijui kuhusu hii tasnia.....filamu inalipa sana ona mchanganuo huu
Kwa mimi kwa sababu vifaa vyakwangu kwa filamu 1 natumia 6mil hadi 7mil mpaka picha nakuwa nayo mkononi....ambazo ni sawa na dvd 2400 hivi, sasa nikuulize swaki mkuu Carter unataka kuniambia siwezi kuuza dvd 2400 au kwa usemi mwingine siwezi kurudisha mil7 kwa muda mchache?
Mimi juzi nimetoa filamu inaitwa omega na kwa kuanza nimeanza kwa kopi 15000 na mimi kwa hapa town siwauzii wachuuzi wadogo wadogo, mimi nauza kwa jumla @1600 kwa dvd kwa hiyo 1&2 kwa jumla ni 3000.
na mpka saa hizi dukani kwangu nimebaki na kopi 1200 tu
Hii picha niliitangaza sana na watu walikuwa wanaisubili siku niliyoitoa huwezi amini....na wala sikutegemea nilichokuwa nakiona kuhusu hii filamu...
 
Safi mkuu kwq kuamka kabla kujapambazuka..na kuelimika sio tu kwenda darasan na kupata A bali ni kuweza kutumia fursa vyema ktk mazingira yanayokuzunguka..keep it up!!!!
 
Kwa hiyo mtitu na yeye si msambazaji?amesambaza kazi kadhaa za kanumba na wengineo wengi, je ananua haki zote za wasanii katika filamu au kuna makubaliano tofauti?mbona hujaliweka hili wazi?
 
Wanajamvi Naomba kujua filamu mtitu aliyoigiza hata moja tuu maana mimi namfahamu kama msambazaji na siyo msanii wa filamu
 
Mtitu, wengi hawajui kuwa wewe ndiye uliyeleta mapinduzi ya Filamu Tanzania na Wasanii wakubwa wasingejulikana bila muongozo wako.

Nikupongeze maana unakwenda kuleta mapinduzi mapya ambayo kwasasa unaweza usieleweke sana na kukuongezea maadui! Umetoa ufafanuzi mzuri sana kwa mwenye akili timamu amekuelewa na unastahili kuungwa mkono.
 
Back
Top Bottom