Mto Kongo na Maajabu yake

Mto Kongo na Maajabu yake

Hebu nisaidieni swali hili jamani Congo DRC ni tofauti na Congo Brazzaville??? Na maraisi wao ni tofauti??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mkuu, ni nchi mbili tofauti na zina watawala tofauti, Congo ya kinshasa ni maarufu kidogo kuliko ile ya pili nadhani umaarufu wao unatokana ni vile unavyotaka, wengine lile vumbi la kusimamisha mambo yetu, waasi, muziki hahahaa sipo serious sana maana nipo Canada ile kitu imeruhusiwa huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
,,,,CONGO INA NEEMA NYINGI SANA WANDUGU,,
AFRICA CJUI TUNAKWAMA WAPI,,,!!?

,,KAMA NI MAOMBI MBONA TUNAOMBA KILA CKU, MUNGU IBARIKI AFRICA MUNGU IBARIKI TANZANIA,,mwe wajameni,
 
Ni nchi mbili tofauti Lily Tony .
DRC hii ni Democratic republic of Congo, na Congo Brazzaville ni nchi Jirani ijulikanayo pia kama "Republic of Congo". Wakati DRC wametawaliwa na ubelgiji, Congo Brazzaville wametawakiwa na Ufaransa, ila zote mbili ni waathirika wa tawala za m dikteta, ingawa kiuchumi DRC ipo hoi zaidi.
BTW Lily Tony wewe ni classmate nunaye kufahamu right? Au ni coincidence ya majina!!
nilitaka kuuliza the same qn mkuu,asnt ,Naomba ukijibiwa unitag pls
 
Ni nchi mbili tofauti Lily Tony .
DRC hii ni Democratic republic of Congo, na Congo Brazzaville ni nchi Jirani ijulikanayo pia kama "Republic of Congo". Wakati DRC wametawaliwa na ubelgiji, Congo Brazzaville wametawakiwa na Ufaransa, ila zote mbili ni waathirika wa tawala za m dikteta, ingawa kiuchumi DRC ipo hoi zaidi.
BTW Lily Tony wewe ni classmate nunaye kufahamu right? Au ni coincidence ya majina!!
Asante,kwa ufafanuzi na maelezo mazuri mkuu! Hahaha! sina uhakika kama ni mimi au majina yamefanana.Classmate wa shule/chuo gn boss?
 
MTO KONGO
Afrika ni moja kati ya mabara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo ni mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile, lakini pia ni mto wa tisa kwa ukubwa duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).



MAAJABU YA MTO KONGO
  1. Mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile (Nile River).
  2. Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
  3. Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
  4. Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
  5. Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
  6. Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
  7. Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
  8. Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
  9. Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
  10. Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.


  • Vyanzo (Sources) [emoji117] Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East African Rift Valley.
  • Urefu (Length) [emoji117] 4700 km
  • Bonde (Basin Cover) [emoji117] 4,014,500 km square.
  • Mdomo wa Mto (River Mouth) [emoji117] Atlantic Ocean
View attachment 1015993



Hata cha mkongo kinapatikana huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom