Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 12
- 14
Mimi ni Mkazi wa Mtaa wa Mazimbu Darajani, Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro, jamani mtaani kwetu huku kumekuwa na changamoto ya mto kujaa na kufurika maji hasa kipindi cha mvua hali inayosababisha maisha ya watu kuwa hatarini.
Wanaokuwa hatarini zaidi ni Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari pamoja na wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Maharangu wanaovuka kwenda kuisaka safari yao ya elimu.
Eneo hilo limekuwa ni korofi kwa muda mrefu, mwaka huu 2024 kipindi cha msimu wa mvua tulipata tabu sana ya kuvuka katika Barabara, maji yalijaa yakaingia mtaani.
Licha ya barabara hii kukarabatiwa baada ya mvua kukata lakini bila kuangalia namna ya kuufukua mto huu ili kuuelekeza mto ufuate mkondo wake ni kazi bure maana mvua zikianza tabu itakuwa palepale na barabara itaharibiwa tena.
Sisi hofu yetu kubwa ni Watoto wa shule wanaovuka kwenda kuisaka elimu yao maisha yao yapo hatarini wanaweza kupoteza maisha kwasababu watoto wengine ni wadogo hasa hawa wa shule ya msingi
Mwaka jana 2023 tumeteseka mno kutokana na tatizo la kujaa maji watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha, kwa ufupi miundombinu ni changamoto kubwa kwetu.
Pia huu mto si kujaa tu kwenye barabara bali ukifurika unajaa mpaka kwenye makazi ya watu wa Mtaa wa Mazimbu, pia yanaenda kujaa mpaka kwenye makazi ya Wafanyakazi wa SUA hii ni mbaya sana maana Watu mnaweza kuwa mmelala usiku maji yakaja kuwasomba.
Kipindi cha mvua watoto wanakosa elimu kutokana na hofu ya kuvuka kwenye maeneo ambayo yanajaa maji.
Serikali kupitia Mamlaka husika Bonde la Wami/Ruvu sisi wakazi wa Mtaa wa Mazimbu Darajani tunaomba kufukuliwa kwa Mto Ngerengere maana umekuwa ni kero kubwa mno, hofu yetu kubwa ni msimu wa mvua zikianza tutakuwa wageni wa nani?tunaomba msaada kabla msimu kuanza
Sisi hata Mbunge wetu tu AbdulAziz Abood akilifanya kwa wananchi wake sisi tutafurahi sana au alipeleke ombi letu kwa viongozi husika sisi wananchi wake tupate kusaidiwa.
Pia soma
~ Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kusafisha Mto Ruvu kuondoa matope na uchafu
~ Wanaofanya uvuvi Mto Ngerengere eneo la Tungi na Kihonda wawe makini, kuna mashimo yaliyochimbwa wakati wa ujenzi wa SGR yana kina kirefu