Mtokeo ya kidato cha nne ni hujuma dhidi ya shule za kata.

Mkuu sijakupata hapo unaposema maswali magumu unakuwa unamaanisha nini na utajuaje kuwa hili swali ni gumu na hili ni jepesi
 

Mkuu kuna watu wanadhani Dr. Ndalichako ni mwalimu. Hivi kuna uhusiano gani kati ya msahihishaji na mtahiniwa ambao una nguvu kuzidi ule wa mtahiniwa na mfundishaji?

Yaani hata kama mtu alikuwa anamuona mwanawe haendi shule anakaa vijiweni, basi akifeli lawama kwa NECTA.

Watanzania wenzangu, NECTA sio baraza la kubalansisha matokeo, NECTA ni kipimo. Huyo mwanzisha mada ubongo wake una hitilafu. Kama haoni tofauti ya shule binafsi na za serikali basi atakuwa hajawahi kwenda shule:

1. Shule binafsi zinafanya assessment kila mwezi. Kila topic inavyoisha kuna mtihani. Shule za serikali ni MID -TERM na TERMINAL

2. Shule binafsi zina walimu committed kutokana na mafao yaliyo bora. Shule za serikali walimu ndio hao mishahara laki 2

3. Shule binafsi wanatoa chakula na usafiri kwa wanafunzi. Serikali haina mpango huo, ni miayo kwenda mbele

4. Ni mwalimu yupi serikalini anajali kama hakumaliza syllabus? Au hili nalo hulioni?

Tuache ujuha wa NDALICHOLISM. Ile ni mahakama, mkosaji anaweza kuwa MTAHINIWA au ALIYEMWANDAA na sio MARKER.
 
Mkuu sijakupata hapo unaposema maswali magumu unakuwa unamaanisha nini na utajuaje kuwa hili swali ni gumu na hili ni jepesi


nikupe mfano mwepesi wa shule za msingi. tuchukulie somo la kiingereza. kuna vipengele vya kuuliza. kuna maswali ya true or false, kuna multiple choice (a,b,cd), kuna matching items, kuna maswali makavu kwa mfano what is climate? kuna maswali ya kufafanua kwa mfano: why do you think it was hard to stop slave trade in East Africa.

maswali ya true or false na yale ya abcd... ni mepesi kuliko yale ya ku define au accounting for....... mimi ni mwalimu. mwalimu mwenyewe anapo tunga mtihani huwa anahisi moyoni mwake ugumu au uepesi wa maswali aliyotunga.
 

NECTA wamekana hilo na wamempa yule mkuu wa shule muda ili athibitishe alichokisema.. Sasa kama ni kweli huyo Mwalimu ana ushahidi aende hata mahakamani.. Otherwise u'r all barkin at a wrong tree..
 
Ila naona kama umeeleza zaidi kuhusu muundo wa mtihani maana maswali kuwa na true or false, matching items, fill the blanks haimaanishi kuwa ni marahisi au magumu, Pia hapo mwisho naona umeeleza nilichokuwa nafikiria kuhusu ugumu, yaani neno ugumu mara nyingi ni (subjective)
Je lingetumika kuwa trick questions unaonaje
 
Ni kweli maana kulaumu NECTA ni sawa na kumlaumu hakimu unaaacha yule aliyekupeleka mahakamani
 

naona tricky qstns ni neno sahihi. huenda mtihani hauku balance ili kuweka uwiano kwa wote. lkn sababu za kufeli ni nyingi. hili tatizo ni pana sana
 
naona tricky qstns ni neno sahihi. huenda mtihani hauku balance ili kuweka uwiano kwa wote. lkn sababu za kufeli ni nyingi. hili tatizo ni pana sana
Umenena kweli maana ufaulu wa mwanafunzi ni mchakato
 
serikali / wizara wana makosa, walimu wana udhaifu pia, baraza la mitihani kama sehemu ya wizara ina makosa, halmashauri zetu / tamisemi, wazazi/ jamii na matumizi mabaya ya tehama na hasa mitandao ya jamii na simu za mkononi. watoto siku hizi hawasomi! mwalimu anafundisha huku mtoto anachat na mwenzake darasani simu ikiwa kwenye vibration. Mungu atusaidie lkn mimi nikipewa wizara ya elimu ili niwe waziri nadhani nitakataa wadhifa huo. ni mzigo ambao haubebeki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…