Mkuu kuna watu wanadhani Dr. Ndalichako ni mwalimu. Hivi kuna uhusiano gani kati ya msahihishaji na mtahiniwa ambao una nguvu kuzidi ule wa mtahiniwa na mfundishaji?
Yaani hata kama mtu alikuwa anamuona mwanawe haendi shule anakaa vijiweni, basi akifeli lawama kwa NECTA.
Watanzania wenzangu, NECTA sio baraza la kubalansisha matokeo, NECTA ni kipimo. Huyo mwanzisha mada ubongo wake una hitilafu. Kama haoni tofauti ya shule binafsi na za serikali basi atakuwa hajawahi kwenda shule:
1. Shule binafsi zinafanya assessment kila mwezi. Kila topic inavyoisha kuna mtihani. Shule za serikali ni MID -TERM na TERMINAL
2. Shule binafsi zina walimu committed kutokana na mafao yaliyo bora. Shule za serikali walimu ndio hao mishahara laki 2
3. Shule binafsi wanatoa chakula na usafiri kwa wanafunzi. Serikali haina mpango huo, ni miayo kwenda mbele
4. Ni mwalimu yupi serikalini anajali kama hakumaliza syllabus? Au hili nalo hulioni?
Tuache ujuha wa NDALICHOLISM. Ile ni mahakama, mkosaji anaweza kuwa MTAHINIWA au ALIYEMWANDAA na sio MARKER.