Mtokeo ya kidato cha nne ni hujuma dhidi ya shule za kata.

mtihani wowote ule lazima ugawanywe katika mfumo ambao kitaalamu unaitwa table of specification (KCAASE). kwa kifupi lazima kuwe na maswali mepesi sana (1/4), maswali ya kati ambayo siyo magumu sana wa rahisi sana (1/2) na maswali mengine magumu sana (1/4). maswali magumu sana yatajibiwa kwa usahihi na watoto wenye akili sana na wanaojituma katika masomo. lengo la mtihani siyo maswali yawe magumu yote ili kuwafelishs watoto. wanaosema pana uwezekano maswali ni magumu sana ili wanafunzi waliopo ktk shule za kata wafeli, wanaweza kuwa sahihi. japo za binafsi zimefelisha lkn siyo kwa kiwango kikubwa sn.

sababu za watoto kufeli kwa asilimia kubwa ni nyingi lkn maswali magumu nadhani ni moja wapo
Mkuu sijakupata hapo unaposema maswali magumu unakuwa unamaanisha nini na utajuaje kuwa hili swali ni gumu na hili ni jepesi
 
Kiongozi, kwa mtazamo wako tatizo ni watunga mitihani na wasahihishaji. huko mashuleni kuko shwari? Tatizo ni mfumo mzima wa elimu na siyo vipandevipande. Mnafikiri leo hii Dr. Ndalichako akiondolewa ndoo mambo yatakuwa shawari la hasha. Serikali inapobabaika hata kuonesha mtaala. Tatizo ni kubwa hata pa kuanzia hapajulikani labda kuunda tume ya kitaalam ya kuchunguza mfumo mzima na sio vipandevipande

Mkuu kuna watu wanadhani Dr. Ndalichako ni mwalimu. Hivi kuna uhusiano gani kati ya msahihishaji na mtahiniwa ambao una nguvu kuzidi ule wa mtahiniwa na mfundishaji?

Yaani hata kama mtu alikuwa anamuona mwanawe haendi shule anakaa vijiweni, basi akifeli lawama kwa NECTA.

Watanzania wenzangu, NECTA sio baraza la kubalansisha matokeo, NECTA ni kipimo. Huyo mwanzisha mada ubongo wake una hitilafu. Kama haoni tofauti ya shule binafsi na za serikali basi atakuwa hajawahi kwenda shule:

1. Shule binafsi zinafanya assessment kila mwezi. Kila topic inavyoisha kuna mtihani. Shule za serikali ni MID -TERM na TERMINAL

2. Shule binafsi zina walimu committed kutokana na mafao yaliyo bora. Shule za serikali walimu ndio hao mishahara laki 2

3. Shule binafsi wanatoa chakula na usafiri kwa wanafunzi. Serikali haina mpango huo, ni miayo kwenda mbele

4. Ni mwalimu yupi serikalini anajali kama hakumaliza syllabus? Au hili nalo hulioni?

Tuache ujuha wa NDALICHOLISM. Ile ni mahakama, mkosaji anaweza kuwa MTAHINIWA au ALIYEMWANDAA na sio MARKER.
 
Mkuu sijakupata hapo unaposema maswali magumu unakuwa unamaanisha nini na utajuaje kuwa hili swali ni gumu na hili ni jepesi

nikupe mfano mwepesi wa shule za msingi. tuchukulie somo la kiingereza. kuna vipengele vya kuuliza. kuna maswali ya true or false, kuna multiple choice (a,b,cd), kuna matching items, kuna maswali makavu kwa mfano what is climate? kuna maswali ya kufafanua kwa mfano: why do you think it was hard to stop slave trade in East Africa.

maswali ya true or false na yale ya abcd... ni mepesi kuliko yale ya ku define au accounting for....... mimi ni mwalimu. mwalimu mwenyewe anapo tunga mtihani huwa anahisi moyoni mwake ugumu au uepesi wa maswali aliyotunga.
 
Mi ninajiuliza swali 1 tu ambalo mpaka sasa halijajibiwa, Inakuwaje mwanafunzi hajafanya mtihani kabisa na alifukuzwa shule na hata siku ya mtihan no# yake ya mtihan ilikuwa wazi lakin baada ya matokeo kutoka unakuta mtu huyo akapata matokeo tnea mzauri tu amefahulu kwa div 3-24 tena na comb imebalance ?

Nisaidien kujibu swali hilo tu alafu nyie wote mnaoitetea NECTA ndio muendelee na hoja zenu mfu.

NECTA wamekana hilo na wamempa yule mkuu wa shule muda ili athibitishe alichokisema.. Sasa kama ni kweli huyo Mwalimu ana ushahidi aende hata mahakamani.. Otherwise u'r all barkin at a wrong tree..
 
nikupe mfano mwepesi wa shule za msingi. tuchukulie somo la kiingereza. kuna vipengele vya kuuliza. kuna maswali ya true or false, kuna multiple choice (a,b,cd), kuna matching items, kuna maswali makavu kwa mfano what is climate? kuna maswali ya kufafanua kwa mfano: why do you think it was hard to stop slave trade in East Africa.

maswali ya true or false na yale ya abcd... ni mepesi kuliko yale ya ku define au accounting for....... mimi ni mwalimu. mwalimu mwenyewe anapo tunga mtihani huwa anahisi moyoni mwake ugumu au uepesi wa maswali aliyotunga.
Ila naona kama umeeleza zaidi kuhusu muundo wa mtihani maana maswali kuwa na true or false, matching items, fill the blanks haimaanishi kuwa ni marahisi au magumu, Pia hapo mwisho naona umeeleza nilichokuwa nafikiria kuhusu ugumu, yaani neno ugumu mara nyingi ni (subjective)
Je lingetumika kuwa trick questions unaonaje
 
Mkuu kuna watu wanadhani Dr. Ndalichako ni mwalimu. Hivi kuna uhusiano gani kati ya msahihishaji na mtahiniwa ambao una nguvu kuzidi ule wa mtahiniwa na mfundishaji?

Yaani hata kama mtu alikuwa anamuona mwanawe haendi shule anakaa vijiweni, basi akifeli lawama kwa NECTA.

Watanzania wenzangu, NECTA sio baraza la kubalansisha matokeo, NECTA ni kipimo. Huyo mwanzisha mada ubongo wake una hitilafu. Kama haoni tofauti ya shule binafsi na za serikali basi atakuwa hajawahi kwenda shule:

1. Shule binafsi zinafanya assessment kila mwezi. Kila topic inavyoisha kuna mtihani. Shule za serikali ni MID -TERM na TERMINAL

2. Shule binafsi zina walimu committed kutokana na mafao yaliyo bora. Shule za serikali walimu ndio hao mishahara laki 2

3. Shule binafsi wanatoa chakula na usafiri kwa wanafunzi. Serikali haina mpango huo, ni miayo kwenda mbele

4. Ni mwalimu yupi serikalini anajali kama hakumaliza syllabus? Au hili nalo hulioni?

Tuache ujuha wa NDALICHOLISM. Ile ni mahakama, mkosaji anaweza kuwa MTAHINIWA au ALIYEMWANDAA na sio MARKER.
Ni kweli maana kulaumu NECTA ni sawa na kumlaumu hakimu unaaacha yule aliyekupeleka mahakamani
 
Ila naona kama umeeleza zaidi kuhusu muundo wa mtihani maana maswali kuwa na true or false, matching items, fill the blanks haimaanishi kuwa ni marahisi au magumu, Pia hapo mwisho naona umeeleza nilichokuwa nafikiria kuhusu ugumu, yaani neno ugumu mara nyingi ni (subjective)
Je lingetumika kuwa trick questions unaonaje

naona tricky qstns ni neno sahihi. huenda mtihani hauku balance ili kuweka uwiano kwa wote. lkn sababu za kufeli ni nyingi. hili tatizo ni pana sana
 
Umenena kweli maana ufaulu wa mwanafunzi ni mchakato
 
serikali / wizara wana makosa, walimu wana udhaifu pia, baraza la mitihani kama sehemu ya wizara ina makosa, halmashauri zetu / tamisemi, wazazi/ jamii na matumizi mabaya ya tehama na hasa mitandao ya jamii na simu za mkononi. watoto siku hizi hawasomi! mwalimu anafundisha huku mtoto anachat na mwenzake darasani simu ikiwa kwenye vibration. Mungu atusaidie lkn mimi nikipewa wizara ya elimu ili niwe waziri nadhani nitakataa wadhifa huo. ni mzigo ambao haubebeki.
 
Back
Top Bottom