Mtoto (6) mwingine aliyepotea juzi, amekutwa kafariki kwenye jumba bovu. Je, ni kwanini Rais asitangaze hali ya hatari (State of emegency)

Hayo yote uliotaja yapo tunayafahamu
swali kwanini yanaongezeka kwa kasi?

Halafu bangi fafanua inahusike hapo?.
1. Idadi ya Ongezeko la watu manake hata na matukio yataongezeka. Kumbuka kwa sasa hivi mawasiliona ni mepesi sana Kidigitali na Biashara nazo ni nyingi. Zipo biashara ovu.
Wapo watu Vijana wengi sana hawana ajira na wanataka maisha mazuri kwa njia za mkato. Huo ni udhaifu na wanaweza kununuliwa kirahisi sana ili wafanye kazi za kikatili kama hizo. Nakumbuka ilitokea kipindi cha nyuma watu wakadanganywa kuhusu ngozi za watu ni biashara. Na kweli wapo watu waliokamatwa wakisafirisha hizo ngozi. Je, mwenye ngozi(Mtu) si aliuawa ndipo ngozi ikapatikana?
2. Bangi ikivutwa inabadili msimamo wa akili. Mtu aliyevuta bangi anaweza kuiona barabara ya lami kama ni mto mkubwa wa maji. Katika hali hiyo mvuta bangi akili inaweza kumtuma afanye jambo ambalo kama asingelivuta hiyo bangi kamwe asingethubutu kulifanya. Wapo wavuta bangi anaweza kulima kwa jembe la mkono ekari moja kwa siku. Mvuta bangi anaweza kumwona mtoto mdogo kama ni mtu mzima (adult) mwenzake na akamfanyia atakachofanya.
 
Dah
 
Ngoja tumuombe Tlaatlaah
Awafikishie ujumbe huko juu
Kuhusu hali hii

Ova
ni muhimu sana kama wazazi na walezi hasa wa watoto wadogo kama huyo daima kua makini, kua karibu na kua na hakika ya usalama wa mtoto...

kucheza na wenzake wengine hakutoshi kukuhakikishia usalama wake kama mzazi au mlezi..

mara nyingi,
life reality forces, zimewaweka watoto wadogo katika mazingira hatarishi mno yasiyo na uhakika wa usalama wa afya lakini maisha yao pia..

siku hizi mtoto wa umri huo, anaweza kutumwa na mzazi wake kwamba eti nenda kacheze na wenzake kwa mama Fulani, wakati huyo mama mzazi anakwenda kuteka maji au kwenye mishe za maisha, huku pakiwa hakuna uhakika wa huyo mama Fulani kwamba yupo au hayupo nyumbani...

hatari na utata zaidi inamkumba mtoto ikiwa kamkosa huyo mama Fulani alikotumwa aende kucheza na wenzake...

alikotumwa kawakosa, nyumbani kwao pamefungwa, Je, mtoto ataelekea wapi katika hali na mazingira hayo tata na hatarishi hivyo?

R.I.P katoto,
Pole sana wazazi wote and we must be careful kuwalinda watoto wetu kuepuka majuto na lawama kwa wasiohusika 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…