Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
1. Idadi ya Ongezeko la watu manake hata na matukio yataongezeka. Kumbuka kwa sasa hivi mawasiliona ni mepesi sana Kidigitali na Biashara nazo ni nyingi. Zipo biashara ovu.Hayo yote uliotaja yapo tunayafahamu
swali kwanini yanaongezeka kwa kasi?
Halafu bangi fafanua inahusike hapo?.
Wapo watu Vijana wengi sana hawana ajira na wanataka maisha mazuri kwa njia za mkato. Huo ni udhaifu na wanaweza kununuliwa kirahisi sana ili wafanye kazi za kikatili kama hizo. Nakumbuka ilitokea kipindi cha nyuma watu wakadanganywa kuhusu ngozi za watu ni biashara. Na kweli wapo watu waliokamatwa wakisafirisha hizo ngozi. Je, mwenye ngozi(Mtu) si aliuawa ndipo ngozi ikapatikana?
2. Bangi ikivutwa inabadili msimamo wa akili. Mtu aliyevuta bangi anaweza kuiona barabara ya lami kama ni mto mkubwa wa maji. Katika hali hiyo mvuta bangi akili inaweza kumtuma afanye jambo ambalo kama asingelivuta hiyo bangi kamwe asingethubutu kulifanya. Wapo wavuta bangi anaweza kulima kwa jembe la mkono ekari moja kwa siku. Mvuta bangi anaweza kumwona mtoto mdogo kama ni mtu mzima (adult) mwenzake na akamfanyia atakachofanya.