Mtoto akiri Mahakamani kubakwa na baba yake ambaye ni Mchungaji wa Kanisa

Mtoto akiri Mahakamani kubakwa na baba yake ambaye ni Mchungaji wa Kanisa

Waadventista Wasabato mnachafuliwa huku njooni majibu tuhuma! Inakuwaje mnawapa uchungaji watu ambao hawajabatizwa?
 
Mchungaji huyo alikuwa ni muumini wa Dini ya Kiislam, alibadili dini na kuanza kuhamia katika Ukristo lakini hakubadili dini.
Alibadili DINI lakini hakubadili DINI
Ndio umeandika nini boss?
 
Hawa wabakaji na watu wanaokula mashoga dawa yao ni kifo ,mahakaman huko wanafanya nini kazi kula ugali na maharage ya bure.
 
View attachment 2392038
Nurdin Abdallah

Shahidi namba moja ambaye ni mtoto wa miaka 6 anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi Mchungaji Nurdin Abdallah (54) na Muinjilisti wa kanisa la waadventista wasabato Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza, amekiri mbele ya Mahakama kufanyiwa kitendo hicho kwa nyakati tofauti na baba yake huyo.

Kesi hiyo ya ubakaji namba 79 ya mwaka 2022, ilifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 12, mwaka huu.

Leo Oktoba 19, 2022 kulikuwa na mashahidi watatu waliotoa ushahidi Mahakamani hapo akiwemo mtoto ambaye ndiye mwathirika.

Imeelezwa kuwa chanzo cha kubaini tukio hilo kuna mwanachama mmoja wa Ustawi wa Jamii alipata taarifa kutoka kwa majirani, wakamtafuta mtoto ambaye alieleza anayofanyiwa na baba yake.

Mtoto akapelekwa Polisi, daktari akaeleza jinsi sehemu za siri za mtoto zilivyotanuka, ndipo taratibu za Mahakamani zikaanza.

Akiwa Mahakamani mtoto alieleza kuwa baba yake amekuwa akimfanyia vitendo hivyo usiku huku akioneshea sehemu zake za siri kwa kutumia mkono wake.

Alipoulizwa kuhusu mama yake alipo akasema hajui alipo kwa kuwa aliondoka.

Mwathirika huyo amesema alimwambia shangazi yake kuhusu anachofanyiwa na baba yake, lakini hakufanya kitu, baadaye baba yake akamnunulia nguo ili asiseme anachofanyiwa, ndipo akaamua kwenda kusema kwa jirani.

Baada ya maelezo hayo, hakimu akampa nafasi baba mtu kumuuliza mtoto, kwanza akaulizwa kama anamtambua, akakiri kuwa huyo ni mwanaye kabisa wa kumzaa.

Mtuhumiwa akaanza kumuuliza maswali mtoto, akamuuliza kama kuna watu ambao wamemtuma aje azungumze hayo Mahakamani, mtoto akasema: "Hakuna aliyenituma nisema haya."

Baba mtu: Kwa hiyo wewe unasema uongo?
Mtoto: Hapana sisemi uongo kwa kuwa kanisani tuliambiwa ukisema uwongo unaenda motoni, mimi naogopa kwenda"

Baba: Unasema mimi nimekubaka, kweli wewe unajua kubaka
Mtoto: Ndio wewe ulinibaka, ulikuwa ukiniingizia dude lako huku (akionesha kwa mkono sehemu za siri)

Baba: Kwahiyo hautaki kuja nyumbani?
Mtoto: Ndio sitaki kwa kuwa wewe utanibaka

Baba: Unataka kuishi wapi?
Mtoto: Nataka kuishi na mama James (ni katika kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu) au mama

Mchungaji huyo alikuwa ni muumini wa Dini ya Kiislam, alibadili dini na kuanza kuhamia katika Ukristo lakini hakubadili dini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4, 2022 na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: EATV

Pia Soma: Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6
Siyo muumini wa Kanisa la Sabato alikuwa mchungaji wa Kanisa la kilokole acha chuki
 
WACHUNGAJI OENI JAMANI.
Mtataguna kondoo mpk mtamaliza kabla mwenye kondoo hajarudi.
Kudadeki.

Au km vipi wale wote wenye imani za kukatazwa kuoa wakatwe MAKENDE jumla. Au watamaliza watoto hawa viumbe
 
Back
Top Bottom