Kwa kawaida kama mtu atazama Kwenye bahari au ziwa au kisima Kuna hoja ya kuzingatia kuwa :-
:baada ya kuzama, mwili unaweza kuanza kuibuka juu ya maji baada ya siku 2 hadi 5,ila itategeneana na gesi zinazojikusanya mwilini wakati wa kuoza.Lakini si kila mwili huibuka haraka — kuna maeneo yenye maji baridi au mtiririko mkubwa ambapo mwili unaweza kuchukua muda zaidi, au hata usionekane kabisa.
Hivyo kwa hoja yako kuwa kwani kisima hicho hakikutumika kwa siku mbili na kumuona huyo mtoto yaweza kujibiwa kuwa huenda mtoto akizama chini na baadae baada ya Hali niliyoieleza hapo juu ,mwili umeibuka
Waafrika na maombi...! hata vitu vinavyohitaji kutumia akili ni kukimbilia maombi! Yaani watu wachimbe kisima nyumbani bila kuweka mazingira ya kulinda watoto wasidhurike eti wategemee maombi....kimsingi hao wazazi ni wajinga na wanastahili wakamatwe Kwa uchunguzi.