MTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA.
Mtoto Leonard Morisha Mwenye umri wa Miaka 11 Mkazi wa kijiji na kata ya Ngemo wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita aliyefariki June 27 ,2017 katika hospitali ya Geita amefufuka baada ya kuzikwa kwa kipindi cha miaka 5 mpaka kufufuka kwake huku ikidaiwa kukatwa ulimi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka.
Kamanda amesema mtoto huyo baada ya kuonekana katika Maduka hayo alikuwepo mlinzi katika Maduka hayo aitwae Emmanuel Busiga alimchukua na kumpeleka kwao badae alifikisha taarifa katika uongozi wa kijiji.
"Mtoto huyo ana afya njema lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi katika kituo cha afya cha Masumbwe alibainika kukatwa ulimi kwa kiwango kikubwa mishipa ya ulimi wake na kusababisha ashindwe kuongea, " Mwaibambe.
Mwaibambe amesema baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la polisi lilipata kibali kutoka katika Mahakama kwa ajili kufukuwa kaburi lake ambalo mtoto huyo alikuwa kazikwa na kukuta kaptura pamoja na suruali ya Baba mzazi wake aliyefariki mwaka 2019.
#KitengeUpdates
View attachment 2047442