Mtoto aliyeibwa Januari 15 apatikana kwenye mashamba ya Miwa

Mtoto aliyeibwa Januari 15 apatikana kwenye mashamba ya Miwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
IMG_2626.jpeg
Mtoto Shamimu Nasibu, mwenye umri wa miaka miwili ambaye aliripotiwa kupotea alipokuwa akicheza na mwenzake karibu na nyumbani kwao, hatimaye amepatikana akiwa hai kwenye mashamba ya miwa katika Kijiji cha Kisanga, kata ya Ruaha, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Mtoto huyo aligunduliwa na wasamaria wema waliokuwa wakipita katika mashamba hayo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Jnuari 19, 2025, baba mzazi wa mtoto huyo, Nasib Ndihagule amesema Shamimu alipatikana akiwa hana nguo, hali inayozua maswali kuhusu nani alimvua nguo hizo na kwa sababu gani.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kupitia taarifa rasmi kuwa mtoto huyo alitelekezwa na watu wasiojulikana katika mashamba ya miwa kwenye kitongoji cha Mhovu yaliyopo Kijiji cha Kisanga.
 
Back
Top Bottom