Mtoto ana mwaka 1 na miezi 4, mama yake ana ujauzito wa mwezi 1

mdada moja ametoka kujifungua jana alipata ujauzito mwanae akiwa na miezi 7 alafu mtoto wa kwanza ilikuwa operation
 
Mi naona hapo jamaa anaogopa operation tu
 
Pole ayse. Mtoto anayenyoa hawezi kupata tatizo lolote, cha msingi hakikisha anapata mchanganyiko wote muhumu hasa maziwa, samaki, matunda n.k. Mama aache kumnyonyesha maana akiendelea atahatarisha afya ya mama na mtotoaliyeko tumboni. Mama aanze kuhudhuria clinic ya uzazi hospitali kumbwa, madaktari specialists wa operation za uzazi waanze kum-attend na kufuatilia kwa makini kadiri mtoto wa tumboni anavyokua. Clinik ni ya muhimu sana maana mshono wa mwanzo wakati mwingi unakuwa haujapona vizuri kwa ndani. Imarisha lishe kwa mama pia ili awe na nguvu na damu ya kutosha ili kuepuka kuongezewa damu wakati wa operation.
 
Hongera na pole.Hongera kwa mkeo kupata ujauzito.Pole kwa mkeo kushika mimba akiwa ametoka kwenye oparesheni.Tumuombe Mungu ampe afya njema mkeo.Juu ya muda wa kupishana usiogope sana, afadhali wewe mimi watoto wangu wawili waliofuatana wamepishana mwaka mmoja!. Mimi nilifanya makosa siku za mwanzo. Kutokana na majukumu nilikuwa mtu wa kusafirisafiri sana.Baada ya kujifungua mke wangu alikwenda kwao.Akamuacha mtoto mkubwa (mwenye mwaka 1) kwa Mama mkwe.Akarudi na kachanga.Nilipata dharura ya kufika kwa wakwe nilimkuta dogo yupo katika hali mbaya ya kiafya (nafikiri viporo, lishe isiyo bora,kutokula kwa wakati n.k.). Fasta nilirudi naye home. Nikasimamia afya yake kikamilifu.Sasa hivi wakubwa tu wapo vizuri sana kiafya.Watu wanawaita mapacha wa nje! Ninakushauri: 1.Ongeza upendo kwa kwa mkeo 2.Dogo aendelee kunyonya kwa ushauri wa daktari 3. Juu ya hali ya operesheni ya mkeo nenda fasta hospitali (waone mabingwa/wataalamu) 4. Ukiweza rudi mapema nyumbani.
 
Mbona mtoto wa mwaka na miezi minne ni mkubwa tu. Mke wangu alipata mimba mtoto wetu wa kwanza akiwa na miezi sita tu.

Mama aliilea mimba na huku akimnyonyesha mtoto wetu wa kwanza hadi alipofikisha miez 12 ndo akamwachisha.

Watoto wote wanaendelea vizuri na wapo shuleni tena ni "majiniaz"

Nakushauri msiitoe hiyo mimba, najua mnawaza kuitoa!!
 
Mke inabidi awe kwa uangalizi wa karibu na dr

Ila ulishindwa kabisa kumwaga nje au kutumia condom?
Mbona hamuwahurumii hao wake zenu????
Hizi mambo huwezi kuzijua kama haupo kwenye ndoa!! Ni ngumu sana kutumia kondomu kila siku na mkeo.

Wengi wamejikuta wakipeana mimba by mistake baada ya utamu kukolea na kushindwa kuchomoa kumwaga nje, na wengine kalenda Method imewapoteza na kujikuta mimba zinaingia by mistake.
 
Mkeo alijifungua kwa kuchinjwa tumboni?
 
Tupo kwenye ndoa miaka chungu nzima.

Hapa swala ni kujali afya na ustawi wa mwenzio tu. Kitu unacho halali yako kuzingatia uzazi wa mpango kwa siku 3 au 4 kwa mwezi unashindwaje?

Mkishindwa condom ktk danger days tu
Sema tu wanandoa wengi hujiendekezq na wanawake ni waoga kuwaeleza wenzao wanavyojisikia kuhusiana na swala hilo kwa kuhofia "kuchepuka"

Kitunze kikutunze Mkuu...
 
Haina shida kabisa, mi Nina Rafiki yng alijifungua kwa operation mtoto akiwa na miez Tisa tuu ikanasa nyingine akamuona Dr wake na akaambiwa hamna shida na hapa tayari kajifungua ana mwezi sasa, nakushaur afike kituo cha afya kama hakuna.complications yeyote atakua salama, jitahidi mtoto apate lishe bora na amwachishe Ku yonya ili na kiumbe cha tumboni kipate haki yake
 
Bila shaka mtoa Uzi utakua MTU wa kanda ya ziwa manake kule ndo mnazaana ovyo ovyo kama kuku
 

kuwa na amani kaka, hakikisha mama anakula vizuri na anaendelea kumhudumia huyo wa kwanza kama kawaida hakuna madhara yoyote, mi wa kwangu alipata mtoto akiwa ana mwaka. na nilikwenda had kwa ma specialist wakaniambia hakuna madhara yoyote
 
Huyu jamaa sijui alishindwa ata kuchepuka ...namuonea huruma mama dahhh
 
Aisee Mkuu, basi sawa ila natamani nionane na huyo mwanamke, Dr akasema hakuna shida kwelii? Basi sawa hongera kwake
 
Hapo ndo tunapo uona umuhim wakuchepuka.
 
Aisee Mkuu, basi sawa ila natamani nionane na huyo mwanamke, Dr akasema hakuna shida kwelii? Basi sawa hongera kwake
Operation za Leo sio sawa na za mama zetu miaka hio, now mambo yamechange
 
Operation za Leo sio sawa na za mama zetu miaka hio, now mambo yamechange
Tofauti ni moja tu sikuhizi hawachani Msalaba yani usawa wa kitovu kushuka chini, sa hv wanapasua tofauti ila maumivu Yale Yale na lazima uzingatie ushauri. Any way ni sawa pia km tushakuwa Wa U.S.A
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…