Mtoto ana Umri wa Wiki Moja na ana Mafua makali Msaada

Mtoto ana Umri wa Wiki Moja na ana Mafua makali Msaada

Black BackUp

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
717
Reaction score
666
Habari,

Mtoto wa Umri wa Wiki Moja ana Mafua makali na anakohoa mara mojamoja... Naomba Ushauri wa kitaalam na namna ya kumsaidia kupata na dawa.

Asante
 
Ephedrine nasal drop

Sent from my iphone 13 pro using JamiiForums mobile app
Mtoto mdogo ni tofauti na wakubwa, hapewi dawa tu ilimradi tuondoa symptoms.

Sawa ephedrine ni nasal decongestant nzuri ila bado hujamtendea haki mtoto. What if kuna tatizo jengine ambapo kama angesaidiwa kuondosha hilo basi ingeondosha vyote hivyo mafua na kifua?
Sasa unafikiri kama ana bronchiolitis au pneumonia, hiyo ephedrine itamfikisha wapi?

Kwenye pediatrics tunasema, "Child is not a small adult" kwamba huwezi kumtibu kama unavyomtibu mtu mzima, eti kwa kuwa ana mafua ndio umpe nasal drop.

Mfano mzuri, watoto wanaopatwa na diarrhoea (kuhara) mara nyingi hupata kutapika sana. Pamoja na kutapika kwake hapaswi kupewa antiemetic (dawa ya kuzuia kutapika). No shortcut. Tibu tatizo kwanza kisha kutapika kutaondoka kwenyewe. Hapo ndio utakua umemsaidia mkuu.

Kisha mtoto ni wa umri wa wiki 1 (siku 7), like serious boss??
 
Black BackUp usitumie hiyo dawa iliyoandikwa hapo juu, itapunguza mafua kwa muda kisha tatizo litarudi tena.

Ni hatari, hasa kwa mtoto wako wa siku 7. Nakuomba umpeleke mtoto hospitali.
 
jitahidi mahali anapolala pasiwe na vumbivumbi (allergy) hivyo waweza chukua uangalifu juu ya godoro, mashuka, mapazia pia mazulia kuhakikisha ni masafi na kubadilisha kila baada ya kuonesha dalili ya uchafu.
 
Asante sana
 
Habari,

Mtoto wa Umri wa Wiki Moja ana Mafua makali na anakohoa mara mojamoja... Naomba Ushauri wa kitaalam na namna ya kumsaidia kupata na dawa.

Asante
Mpake mafuta ya nazi kuzunguka pua yake karibu na matundu inasaidia kulainisha mafua yatachuruzika apate kupumua vizuri yakikauka unampaka tena.Hii itasaidia aweze kunyonya na kadri ananyonya sana ndo tiba nzuri ya mafua kupona.

Akibanwa na mafua anashindwa kunyonya so ikishindikana mpeleke hospital
 
Back
Top Bottom