Pamoja na kejeli ulizopewa ila nakushauri; Badili huo muda wa kumlisha chakula. Jitahidi pia saa 3-4 usiku mpe chakula. Halafu, ni chakula gani?? Isije kuwa ni uji unasema chakula. Mpe kitu kigumu kidogo kikae tumboni. Pia, jitahidi asilale na wewe karibu. Hivi umewahi jiuliza, ukiugua ukalazwa utafanyaje?? Najua maisha magumu ila jitahidi awe na kitanda chake mwenyewe. Kama upo na baba tu yaani huyo ka ni wa kwanza mpe baba ambembelezee kwa kitanda chake hadi usingizi ndio arudi sehemu yake kulala