Mtoto anarithi akili ya kuzaliwa kwa baba au kwa mama?

Ilambo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
475
Reaction score
89
Habari wana Jf,

Nauliza katika kutungwa kwa mimba akili ya kuzaliwa na ya darasani (intelligence) mtoto anaridhi kwa baba au kwa mama?

Tafadhali majibu ya kitaalamu.
 
Safest bet ili awe sharp kichwani ni mazingira tu unayomuandalia mwanao. Kuanzia mimba inapotungwa, mama inabidi awe stress-free na apate mahitaji yote muhimu. Lishe ni muhimu sana, miezi 6 ya mwanzo mtoto hatakiwi kugusa chochote zaidi ya maziwa ya mama yake, hata maji ya kunywa hayatakiwi. Akishavuka miezi 6 nadhani ndio anaweza kuanza kusagiwa mchanganyiko wa vyakula kama ndizi na samaki, viazi. Sembe na wali mwiko.

Akishafikisha miaka miwili nadhani ndio anaweza kukamua chochote, kwa sababu msingi utakuwa tayari umeshajengwa. Hii mambo aliniambia m'dingi kipindi flani so kuna vingine nimesahau, nitamuuliza fresh nikiwa tayari kufanya mambo.

Nadhani ukizingatia hayo, hata kama mama na baba mnatoka kizazi flani 'amaizing' na cha 'great thinkers', dogo atakuwa poa tu.
 
Habar wana jf,nauliza ktk kutungwa kwa mimba akili ya kuzaliwa na ya darasani(intelligence) mtoto anaridhi kwa baba au kwa mama?? Tafadhar majibu ya kitaalamu....
It is a game of probability,inachukua popote;kwa mama,baba,bibi au babu wa pande yoyote hadi kizazi cha tano nyuma ndo mwisho
 
Nilishajaribu kufanya research juu ya suala hilo, kwa kusoma vitabu, kudadisi kwenye internet na kufanya tathmini kwa baadhi ya watu niwajuao, nikaona kwenye vitabu au makala nyingi wameandika kuwa, kisayansi, it has been proved that, about 80 percent of a child's intelligence anarithi kwa mama. Then percent nyingine iliyobaki inategemea na lishe, mazingira, akili ya baba etc. Then nikafanya uchunguzi kwa baadhi ya watu niwajuao, kwa kuangalia background za wazazi wao, nikagundua ni kweli, mtoto anarithi asilimia kubwa ya IQ yake kutoka kwa mama.
 
Kuna madhara eyote mtot wa mwez 1na nusu kupatiwa maj yakunywa??? Msaada kidogo hapa wakuu
 
Mmmnnnhhhhhhhh.

Dogo langu uko vizuri eh.

Ila mdingi alianzaje anzaje kukuambia?
 
Mmmnnnhhhhhhhh.

Dogo langu uko vizuri eh.

Ila mdingi alianzaje anzaje kukuambia?


Hahaha, tulianzia kwenye story tu kama baba na mwanae, kama wanaume, na pia kama washkaji. Nadhani tulikuwa tunacheki documentary ya barefoot bandit kwenye tv. Dogo alikuwa anaiba ndege na boats ndogo na anazi-control kwa kusoma manuals na uzoefu wa kucheza video games. I was impressed by the dude, ndio katika kumjadili tukafika huko.
 

Ah,ok. Thought I had a nephew or niece somewhere na siambiwi.
 
Ah,ok. Thought I had a nephew or niece somewhere na siambiwi.


Hahaha, alinipa shule kubwa kinoma, nikiweka hapa haitoshi. Imenifanya hadi leo hayo masuala nayachukulia serious sana, so i won't go around making random babies with random chicks. Nahitaji kufanyia kazi vitu vingi sana, sana, na itachukua muda.
 
Mtoto akiwa na akili ujue karithi toka kwa baba, akiwa mjinga ujue umetoka upande mwingine.
 
Mtoto anarithi kote ndio maana magonjwa ya kurithi huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumpata mtoto endapo wazazi wake wote wana asili ya magonjwa Hayo kwa karibu na huwa na uwezekano mdogo wa kuyarithi endapo hata mzazi mmoja tu atakuwa Hana asili ya kuwa nayo.

Ila kuna factor zinazocontrol mambo mengine katika kurithi kwa mtoto mfano swala akili kuwa nyingi kwa mtoto ambazo zinarithiwa kwa upande wa Mama. Endapo Mama Ana asili ya ukilaza, mtoto itabidi awe katika mazingira yatakayomchochea kuwa na akili nyingi.

Mambo mengine ni Mpishano wa umri wa Baba na Mama, Kuchelewa kuzaa kwa Mama, umri wa Baba alieitia mimba na afya yake mama kipindi cha ujauzito pia humfanya mtoto apate athari ambazo wakati mwingine huweza kutafsiriwa kuwa alirithi kwa Mama wakati kiuhalisia ni athari zilizotokana na mambo mwingine.
 
akili hairithiwi wandugu kila binadamu anaumbwa na akili yake separate
 
Habari wana Jf,

Nauliza katika kutungwa kwa mimba akili ya kuzaliwa na ya darasani (intelligence) mtoto anaridhi kwa baba au kwa mama?

Tafadhali majibu ya kitaalamu.

Mbona swali la ajabu hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…