Safest bet ili awe sharp kichwani ni mazingira tu unayomuandalia mwanao. Kuanzia mimba inapotungwa, mama inabidi awe stress-free na apate mahitaji yote muhimu. Lishe ni muhimu sana, miezi 6 ya mwanzo mtoto hatakiwi kugusa chochote zaidi ya maziwa ya mama yake, hata maji ya kunywa hayatakiwi. Akishavuka miezi 6 nadhani ndio anaweza kuanza kusagiwa mchanganyiko wa vyakula kama ndizi na samaki, viazi. Sembe na wali mwiko.
Akishafikisha miaka miwili nadhani ndio anaweza kukamua chochote, kwa sababu msingi utakuwa tayari umeshajengwa. Hii mambo aliniambia m'dingi kipindi flani so kuna vingine nimesahau, nitamuuliza fresh nikiwa tayari kufanya mambo.
Nadhani ukizingatia hayo, hata kama mama na baba mnatoka kizazi flani 'amaizing' na cha 'great thinkers', dogo atakuwa poa tu.