Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,375
akili hairithiwi wandugu kila binadamu anaumbwa na akili yake separate
Mkuu, hiyo ni mpaka kwa Wanyama kama mbwa, farasi n.k Unadhani kwanini Serikali inaagiza mbwa nje wakati hapa wapo wa kwetu wa kuokota tu? Unadhani kwanini kuna familia wamejazana vilaza na nyingine wanaongoza kielimu mpaka wanaudhi?
Ukiachana na factor ya mazingira yanayochochea akili kukua, kuna swala la kurithi, ndio maana kuna mtu mmoja anakesha darasani anapata division one ya point 9 wakati kuna mwanafunzi anasoma kiasi, anacheza mpira sana na bado anapata division one ya point 9 pia. Kuna watu naowajua Mimi ambao waliwahi kuamua kuinclude masomo ambayo wengine walisoma miaka 4 wiki 3 kabla ya finals na wakafaulu kuliko wote.
Sio hadithi, kuna utofauti katika uwezo wa kujifunza kitu na kukaa nacho kichwani kwa muda mrefu. Kuna watu wana uwezo mkubwa wa kuelewa kitu haraka sana ila pia wana memory ya Samaki na wanashau haraka pia. Pia kuna watu wanajifunza haraka sana na kuelewa kwa muda mfupi sana na hakitoki hata miaka 2 ipite, Sasa hiyo siyo swala la hivi tu, ni kizalia.
Lakini pia, unapaswa kuelewa kuwa swala la àkili ni pana sana na si katika maswala ya darasani tu kwa sababu maarifa kwa ujumla wake ni mengi sana na si kila mtu anaeyaweza yote. Kuna genius wa Kutumia vyombo vya muziki, kuna genius wa kubuni kemikali za kudhuru, kuna genius wa kuiba, kuna genius wa fizikia, kuna genius wa upasuaji, magenius wa uongo, genius wa mapigano, genius wa kutumia silaha, genius wa kuunda mashine, genius wa lugha, genius wa kuchora, na mwingine mengi na yote haya yanaendeshwa na genetics ambazo ni vinasaba vinavyorithiwa na hata kama hujajua bado kuwa uwezo wako ni upia, haina maana kuwa havipo ndani yako.
Mleta mada kachokoza mada pana sana ila hajui tu.