Mtoto anarithi akili ya kuzaliwa kwa baba au kwa mama?

akili hairithiwi wandugu kila binadamu anaumbwa na akili yake separate

Mkuu, hiyo ni mpaka kwa Wanyama kama mbwa, farasi n.k Unadhani kwanini Serikali inaagiza mbwa nje wakati hapa wapo wa kwetu wa kuokota tu? Unadhani kwanini kuna familia wamejazana vilaza na nyingine wanaongoza kielimu mpaka wanaudhi?
Ukiachana na factor ya mazingira yanayochochea akili kukua, kuna swala la kurithi, ndio maana kuna mtu mmoja anakesha darasani anapata division one ya point 9 wakati kuna mwanafunzi anasoma kiasi, anacheza mpira sana na bado anapata division one ya point 9 pia. Kuna watu naowajua Mimi ambao waliwahi kuamua kuinclude masomo ambayo wengine walisoma miaka 4 wiki 3 kabla ya finals na wakafaulu kuliko wote.
Sio hadithi, kuna utofauti katika uwezo wa kujifunza kitu na kukaa nacho kichwani kwa muda mrefu. Kuna watu wana uwezo mkubwa wa kuelewa kitu haraka sana ila pia wana memory ya Samaki na wanashau haraka pia. Pia kuna watu wanajifunza haraka sana na kuelewa kwa muda mfupi sana na hakitoki hata miaka 2 ipite, Sasa hiyo siyo swala la hivi tu, ni kizalia.
Lakini pia, unapaswa kuelewa kuwa swala la àkili ni pana sana na si katika maswala ya darasani tu kwa sababu maarifa kwa ujumla wake ni mengi sana na si kila mtu anaeyaweza yote. Kuna genius wa Kutumia vyombo vya muziki, kuna genius wa kubuni kemikali za kudhuru, kuna genius wa kuiba, kuna genius wa fizikia, kuna genius wa upasuaji, magenius wa uongo, genius wa mapigano, genius wa kutumia silaha, genius wa kuunda mashine, genius wa lugha, genius wa kuchora, na mwingine mengi na yote haya yanaendeshwa na genetics ambazo ni vinasaba vinavyorithiwa na hata kama hujajua bado kuwa uwezo wako ni upia, haina maana kuwa havipo ndani yako.
Mleta mada kachokoza mada pana sana ila hajui tu.
 
Saikolijia inasema akili hailithiwi, kila mtoto anazaliwa akiwa empty kichwani then anaanza kujifunza baada ya kuzaliwa, hivo ni juu ya mzazi kumjenja mtoto kiakili.
 
Hahaha, alinipa shule kubwa kinoma, nikiweka hapa haitoshi. Imenifanya hadi leo hayo masuala nayachukulia serious sana, so i won't go around making random babies with random chicks. Nahitaji kufanyia kazi vitu vingi sana, sana, na itachukua muda.


Aisee bro...inabidi ufungue thread!

Mtoto akiwa na akili ujue karithi toka kwa baba, akiwa mjinga ujue umetoka upande mwingine.

Hahahahahaha...hivyo tu yani!
 
Nimekumiso pia, kwa sasa nipo nimeshamaliza kuvuna mihogo kule kijijini.

hongera ndio maana umekaa kimya unakula hogo lako la jang'ombe. nitakutafuta pm tusijechakachua topic ya watu ikawa shidaa
 
Wakati wengine bongo wakiangalia "namna" ya kuwadedisha madingi zao ili warithi Mali wengine wanaangalia Akili haha ha Akili mwachie cc miss chagga
 
Last edited by a moderator:
Saikolijia inasema akili hailithiwi, kila mtoto anazaliwa akiwa empty kichwani then anaanza kujifunza baada ya kuzaliwa, hivo ni juu ya mzazi kumjenja mtoto kiakili.

Unachosema ni kweli Momy, ila tunazungumzia uwezo wa mtu kukielewa kitu,Kuprocess information, kushika na kukitumia kile anachojazwa baada ya kuzaliwa akiwa empty. Tunazungumzia mtu kuwa na uwezo wa kusolve Calculus na kupata huku akiwa anacheza drafti na mpinzani mwenyewe uwezo mkubwa.
Hatuzungumzii uwezo wa mtoto kuikariri periodic table akiwa na miaka 5.
Tunazungumzia uwezo wa mtu kusoma the Guardian lote kwa nusu Saa na kuyarudia yote yaliyomo humo neno kwa neno kwa muda wa miezi mitatu mbele. Huo uwezo hauko kwa kila mtu na hauko conditioned.
 

Nimekuelewa vema, Asante
 
Hivi maana halisi ya akili ni nini ??? Ni uwezo tu wa kusoma gazeti la the guardian na kukumbuka miezi mitatu mbele ??
Kwa mfano Mimi ni mkulima badala ya kulima mpunga Dodoma nikalima mpunga kwenye bonde la mto ruvu sio akili hiyo ?? Kama ndio hivyo je nahitaji kuwa nimerithi kutoka kwa baba au mama ??
Naomba msaada wenu wakuu
 

Hapa ni kweli asilimia 95...
 

Mtoto anarithi pande zote mbili katika uwiano sawa (50%) ila kuna chembe nyingine ambazo huwa zitawala (dorminant genes). Nahisi kama intelligence ni moja wapo. Kwa hiyo, mtoto anaweza kuonekana kuwa na akili kama mzazi mmoja kwa sababu hiyo gene ya intelligence inaimeza ile ambayo iko weak.

Ulichokieleza hapo ni nguvu ya mazingira katika kuimarisha genes (environmental influence on genetic factors). Pia umeeleza mambo yanayotokea kabla ya mtoto kuzaliwa ambayo yanaangukia kwenye kitu kinaitwa epigenetic influence on genes. Hii inatokea kwa sababu kuna baadhi ya proteins zinazowezesha genes kufanya kazi yake.

Ni somo pana ila kama kuna mtu anataka zaidi tuwasiliane!
 


You are wrong 100% mama!
 


Asante Boss, nadhani hii elimu inaihitajika kwa wengi, kama hutajali ianzishie uzi kabisa Chief.

Cc Mentor
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…