Duh, kumbe kweli ni tatizo aisee, wa kwangu muda wa kula ni ugonvi yaani karibu mtaa mzima ujue maana natumia nguvu kumlisha na mpaka sasa mtoto anapenda samaki na juice tu! Ushauri wa kitaalamu nilioelezwa haujanisaidia ingawa najitahidi kuutekeleza, Mama yangu kanisisitiza niendelee kumlazimisha vinginevyo itakula kwangu!
Kuna mdau kasema wa kwake pia anapenda samaki tu, najiuliza inakuwaje maana hata kwa kwangu kwa samaki hakuna haja ya kumlazimisha japo samaki wa dar siwapendi kweli! Mara tunaambiwa wana sumu yaani utatautata tu! Wenye uzoefu zaidi karibuni kwa ushauri zaidi!