Mtoto apendi kula, je mbinu gani itumike apende kula?

Mtoto apendi kula, je mbinu gani itumike apende kula?

Duh, kumbe kweli ni tatizo aisee, wa kwangu muda wa kula ni ugonvi yaani karibu mtaa mzima ujue maana natumia nguvu kumlisha na mpaka sasa mtoto anapenda samaki na juice tu! Ushauri wa kitaalamu nilioelezwa haujanisaidia ingawa najitahidi kuutekeleza, Mama yangu kanisisitiza niendelee kumlazimisha vinginevyo itakula kwangu!
Kuna mdau kasema wa kwake pia anapenda samaki tu, najiuliza inakuwaje maana hata kwa kwangu kwa samaki hakuna haja ya kumlazimisha japo samaki wa dar siwapendi kweli! Mara tunaambiwa wana sumu yaani utatautata tu! Wenye uzoefu zaidi karibuni kwa ushauri zaidi!
Samaki anapend kwa sababu mnaweka chumvi
 
kwa hali hii napata ushawishi kufungua high quality children daycare center,ili watoto walelewe na wakuzwe katika misingi sahihi ya malezi na makuzi
Mkuu sijaelewa kwanini umenikot toa ufafanuzi wa tatizo la mwanangu
 
Ulianza kumpa chakula akiwa n miez mingapi?jaribu kutokumpa vyakula vya sukar.uji wekea karanga midogo zilizosagwa wek chumvi.Watot weng wanapenda ladha ya chumvi
Miez 7 alikuwa anakula ndizi, pia maboga
 
Nimeshukuru umesema "licha ya kumbadilishia chakula mara kwa mara" kwa kuwa wazazi wengi hasa wa mjini kazi yao ni kumlisha mtoto uji wa lishe masaa yote kiasi kwamba unamkifu mtoto.
 
Mpe matunda sana.Wakat wakul usimpe chakula wew mzaz wake.Kama kunawatot wa jiran waite wale nae na ikibid uwawekee sahan moja
 
Pia inashauriwa tuwe na utaratibu wa kubadilisha vyombo tutumiavyo kuwapa watoto chakula, sio mtu unakuwa na bakuli moja au mbili rangi moja ndio vyombo vya kumpa mtoto chakula, mtoto anakinai chakula unaweza kuta kuna siku alikuwa hajisikii vizuri ukampa chakula akala akatapika hii inakaa akilini mwake, sasa unapochukua tu bakuli na kumsogelea kabla hata hujampa chakula anaanza kulia na kukataa kupokea chakula kwa sbabau akili yake inamrudisha kwenye matatizo, huwa inatokea unapompakata ukampa chakula anagoma na kulia lakini unapo mlazimisha akapokea kijiko cha kwanza ananyamaza na kuendelea kula, hapo anakuwa ameonja ladha tofauti na ile siku alipo tapika, huenda siku ile alikunywa uji, basi anapoona ile bakuli anajua ni uji kumbe leo umeweka mtori au chakula kingene, so tunashauriwa kubadili vyombo vya rangi tofauti tofauti kwenye kumlisha mtoto.
 
Ni mtoto wa kiume, ndio anatimiza mwaka mmoja. Hapendi kula, licha ya kumbadilishia chakula mara kwa mara. Mama yake humlazimisha kula angalao vijiko viwili.
kama haya unayosema ni kweli
Nitafute PM Mkuu
Kuna Unga ambao mtoto akipata uji wake siku moja, ya pili anakula kama kawaida,
ni tatizo la kawaida
Nipem namba
Unga ni TZS 5000 kilo moja
 
Pole sana mkuu, ni tatizo la kawaida mtoto kusumbua kula, niliwahi kusoma mahali kwamba njia rahisi ya kumfanya mtoto apende kula ni kutengeneza mazingira ya wakati wa kula yawe kama mchezo Fulani, inafahamika watoto wanapenda sana michezo,kama umri wake unaruhusu unaweza kumwambia ukimaliza kula tutacheza ( Hapa mzee inabidi wewe na wife mara moja moja muwe Mr,Bean!) kuna wadau walijaribu wanasema kuna improvement kwenye kula,hoja ya msingi hapa ni kutokufanya muda wa kula uwe muda wa mapambano,mtoto anakuwa defensive na ana perceive kwamba kula ni kama adhabu au ugomvi.
 
Nilipata tatizo hilo kwa mwanangu kwa muda mrefu,tulihangaika kwa kipindi kirefu hospital tofauti tofauti bila kupata nafuu,namshkur muumba kuna siku mimi mwenyewe nilipata wazo la kumpa mafuta ya samaki ndio ikawa dawa,tafadhali nawe jaribu kumpa hwenda yakamsaidia.
Hiyo dawa inaitwa "COD LIVER OIL"
tafadhali nunua ile ya seven seas ambayo ndiyo bora zaidi japo bei yake iko juu kidogo kulinganisha na nyengine.
 
Wa kwangu anapenda sana machungwa Na matikiti, na nyama, lkn ugali mpaka kumlazimisha
 
Mama asimpe chakula,kikiwa tayari Mara nyingi alishwe na mdada Wa kazi au mdada atoke na mtoto alipo mama yake wakakae chumba/sehemu ingine amlishe atakula tu nine experience hill kwangu
 
Mpe mafuta ya samaki yale 'Seven Seas' utaona mabadiliko

Vyakula mkipika changanya vitu vingi vyenye virutubisho afu mblendie
Mf: ndizi, karoti, hoho, kitunguu, maziwa, mchicha, dagaa/samaki

Hata akila kidogo kidogo unahakika kapata kitu
 
Ila kama mzazi tumia kila njia
-kukaba
-kuimba nyimbo (za chekechea zile)
- kumuacha acheze, unakuwa unamfuata alipo unamlisha kijiko, then akimeza unamfuata tena
-kumlishia nje anakuwa anashangaa shangaa vindege, miti, kunguru
 
Ila kama mzazi tumia kila njia
-kukaba
-kuimba nyimbo (za chekechea zile)
- kumuacha acheze, unakuwa unamfuata alipo unamlisha kijiko, then akimeza unamfuata tena
-kumlishia nje anakuwa anashangaa shangaa vindege, miti, kunguru
kama ni mtumishi je?atayafanya hayo sangapi?nadada wa kazi hatakuwa na muda wa kuyafanya hayo yote pia.wazazi wengi hatuna elimu ya malezi na makuzi inayo muandaa mzazi kumlea ma kumkiza mtoto toka umri 0hadi miezi6,Miezi 6hadi miaka 2,Miaka 2hadi miaka5.na miaka 5-10,10-17.
 
Wa kwangu walikua matwins, yaan huyo mmoja alkua anasumbua sana kula mama yake ana kabana nae hata lisaa hadi nilikua najiskia vibaya wakati analishwa na wanavyochafuana na mama yake, now wana miaka mitatu anakula mpaka umwekee breki anaweza akavimbiwa aisee, mwenzie sa hv anasumbua kiasi, ila sasa kuna mwingine wa miezi minne hata ziwa la mama yake hataki kuliona,
Kwa hiyo kusumbua kwa watoto kula ni jambo la kawaida sana ila inabidi mzazi asizembee hasa kumpotezea kumlazimisha mtoto kula anapogoma.
 
Acha kapigwe njaa ukikapa msosi katakula tuuh..!
 
Back
Top Bottom