Mtoto kapaliwa chakula na kuziba njia ya hewa,mtoto atapona?

Mtoto kapaliwa chakula na kuziba njia ya hewa,mtoto atapona?

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
Heshima kwenu wakuu.
kuna mtoto wa rafiki yangu ana miaka kama mitatu amepaliwa au alibanwa pua ili ameze chakula , chakula kikabana njia ya hewa..
_Hali kama hii ikitokea huwa inakuweje?kwani tunavyoongea mtoto amewekewe oxgen na yupo ICU.
_Namuonea huruma sana Mungu amponye upesi
 
Muingize vidole kooni umtapishe haraka...hata akimeza na kukwama na mwiba wa samaki fanya hivyo
 
kama ameshaperekwa hospital hakuna shida ila huo utaratibu wa kumlisha mtoto huku unambana pua huwa nauchukia sana mim,kwani madhara yake ndio kama hayo,ila dogo atapona tu maana mi niliwahi kuona mtoto aliingiza miambili puani ikatolewa hospital,
 
Yaani huu ulezi mwengine hatari mno![/QUOTE
Sio ulezi ,short cut za kulisha watu wanafikiri mtoto utamlisha kwa dakika mbili,lazima uiweke at least an hour ,mtoto anaweza akawa hakipendi chakula inabidi um cajole.
Hizi short cut zao watatuulia wajomba!
 
Atapona..
Heshima kwenu wakuu.
kuna mtoto wa rafiki yangu ana miaka kama mitatu amepaliwa au alibanwa pua ili ameze chakula , chakula kikabana njia ya hewa..
_Hali kama hii ikitokea huwa inakuweje?kwani tunavyoongea mtoto amewekewe oxgen na yupo ICU.
_Namuonea huruma sana Mungu amponye upesi
 
Mungu mkubwa anaendelea vizuri leo na ametolewa oxgen na mirija mingine ila bado yupo ICU
 
Poleni sana
Kuna mtoto wa ndugu yangu akiwa mdogo nadhani umri wa kutambaa basi aliweka punje ya harage puani kutoka ikawa tabu sana.

Wajuzi wakashauri utafutwe ugoro !
Halafu akavutishwa halafu tundu la pua lisilo na punje ya harage likazibwa alipotaka kupiga chafya likatoka.

Huyo akiwa nyumbani angepewa ugoro lakini yuko Hosp atapona.
 
Acheni kuwalisha watoto vitu vyenye mbegu, au mchele au pipi..sometimes ikishaziba viriba vya hewa basi matibabu yake ni ndani ya dakika tatu tu...ikizidi hapo mtoto anakata roho. Ukimuhasisha hospital atatobolewa sehemu ili aweze kupumua.
 
Back
Top Bottom