pancras utenga
Member
- May 25, 2016
- 68
- 51
Habarini wadau, nina mtoto wangu now anamiaka miwili ila tangu kukua kwake amekua kila akicheka sana anapata kwikwi, shida itakuwa nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana wala hatukuwahi fanya kabisa hiyo michezoKwanini mlikuwa mnamtekenya itotoni kulazimisha atabasamu?
Ikimshika huwa tunampa maji ikata, na sio kila akicheka mara kwa mara ila huwa akicheka sana na muda inamshikaHuu Uzi umenikumbusha mbali Those Days nikiwa Darasa la 3 - 6 week ilikua haipiti bila kuparamiwa na kwikwi Monday to Monday ni Kucheka mpka mbavu zinauma.
Kwa uzoefu wangu Dawa ya kwikwi ni Maji
Tulishajaribu kupata ushauri wa kitaalam hospital ila wanasema yawezekana wakati anazaliwa alilia kwa muda mrefu may be inaweza ikawa chanzo na kusema itaishaga tu, lkn naona now ni 2 yrs no changes, ndo nikaona nije humuMpeleke hospital ukapate ushauri wa kitaalamu..mtoto Hadi anafikia miaka miwili na hari hiyo huogopi mkuu
Habarini wadau, nina mtoto wangu now anamiaka miwili ila tangu kukua kwake amekua kila akicheka sana anapata kwikwi, shida itakuwa nini?
Ahsante sana comrade nimekuelewaKwikwi (hiccups) ni mtetemo usiyo wa hiari wa kiwambo/msuli wa upumuaji [diaphragm] (involuntary diaphragmatic spasms).
Wakati wa kuvuta hewa ndani
kiwambo/msuli wa upumuaji hushuka na kamba za sauti (vocal cords) hufunguka ili kuruhusu hewa kuingia. Mtetemo huo ukitokea wakati wa kuvuta hewa ndani husababisha kamba hizo (vocal cords) kufunga ghafla na kutoa sauti ya "kwi" au "hic" ili kuzuia hewa isiendelee kuingia ndani/kwenye mapafu.
View attachment 3227168
Kiwambo/msuli wa upumuaji (diaphragm), vocal cords/glottis
Kwikwi (hiccups) husababishwa na vitu vingi mfano kumeza hewa nyingi (aerophagia) hasa mtu anapocheka au akila/akimeza haraka haraka.
Hewa ikiingia tumboni kwa wingi hutekenya msuli wa upumuaji [diaphragm] na kuifanya iteteme (spasms) wakati wa kuvuta hewa ndani [kwani yenyewe hushuka kuelekea chini] hivyo kufanya kamba za sauti (vocal cords) kufunga ghafla na kutoa sauti ya "kwi" au "hic" yaani kwikwi/hiccups.
Kwa hiyo kwa mwanao tayari kichocheo/kisababishi (kucheka) kinajulikana.
Aina hii ya kwikwi ya mwanao ni ya muda mfupi tu (transient hiccups) ambayo haihitaji matumizi ya dawa katika kuishughulikia ukilinganisha na kwikwi sugu (chronic hiccups) ambayo huhitaji matumizi ya aina fulani za dawa kuitibu.
Mwanao anaweza akatumia mojawapo ya mbinu hizi pale anapopata kwikwi:
-anywe maji
-ashikilie pumzi na kufumba macho kwa sekunde 15 na kisha kupumua kawaida
-ameze limao
-apulize puto
-akae kwa kuchuchumaa na magoti kugusa kifua
Kila la kheri.