Kwikwi (hiccups) ni mtetemo usiyo wa hiari wa kiwambo/msuli wa upumuaji [diaphragm] (involuntary diaphragmatic spasms).
Wakati wa kuvuta hewa ndani
kiwambo/msuli wa upumuaji hushuka na kamba za sauti (vocal cords) hufunguka ili kuruhusu hewa kuingia. Mtetemo huo ukitokea wakati wa kuvuta hewa ndani husababisha kamba hizo (vocal cords) kufunga ghafla na kutoa sauti ya "kwi" au "hic" ili kuzuia hewa isiendelee kuingia ndani/kwenye mapafu.
View attachment 3227168
Kiwambo/msuli wa upumuaji (diaphragm), vocal cords/glottis
Kwikwi (hiccups) husababishwa na vitu vingi mfano kumeza hewa nyingi (aerophagia) hasa mtu anapocheka au akila/akimeza haraka haraka.
Hewa ikiingia tumboni kwa wingi hutekenya msuli wa upumuaji [diaphragm] na kuifanya iteteme (spasms) wakati wa kuvuta hewa ndani [kwani yenyewe hushuka kuelekea chini] hivyo kufanya kamba za sauti (vocal cords) kufunga ghafla na kutoa sauti ya "kwi" au "hic" yaani kwikwi/hiccups.
Kwa hiyo kwa mwanao tayari kichocheo/kisababishi (kucheka) kinajulikana.
Aina hii ya kwikwi ya mwanao ni ya muda mfupi tu (transient hiccups) ambayo haihitaji matumizi ya dawa katika kuishughulikia ukilinganisha na kwikwi sugu (chronic hiccups) ambayo huhitaji matumizi ya aina fulani za dawa kuitibu.
Mwanao anaweza akatumia mojawapo ya mbinu hizi pale anapopata kwikwi:
-anywe maji
-ashikilie pumzi na kufumba macho kwa sekunde 15 na kisha kupumua kawaida
-ameze limao
-apulize puto
-akae kwa kuchuchumaa na magoti kugusa kifua
Kila la kheri.