Mtoto kula udongo sio jambo la ajabu,ni jambo la kawaida.Isipokuwa inawezekana ana upungufu wa madini fulani mwilini.Unatakiwa kuhakikisha kwamba mtoto wako anapata chakula ambacho ni bora,yaani chakula chenye virutubisho vyote.Kama huna uhakika wa chakula hicho, muona Daktari wa watoto aliye karibu nawe akupe ushauri.Mwisho hakikisha unampa mtoto wako dawa za kutoa minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu.Halafu chuma kumbuka udongo na mchanga ni vitu viwili tofauti.Nadhani mtoto wako anakula udongo,sio mchanga!