Mtoto kutumia muda mwingi shuleni, inasaidia au inabomoa nidhamu yake?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya shule za msingi na zile za awali zikiongezeka, hiyo imeendana sambamba na ongezeko la ratiba ya masomo kwa wanafunzi.

Zamani ilizoeleka wanafunzi wanaotumia muda mwingi shuleni ni wale wanaosoma bweni, lakini hivi sasa hata wale wanaosoma ‘day’ pia wanatumia muda mwingi wakiwa shuleni katika masomo.

Unadhani mwenendo wa wanafunzi wengi hasa wale wa shule za awali na msingi kuutumia muda wao mwingi shuleni, inasaidia nidhamu yake nje ya masomo kuwa nzuri au inambomoa?

=============================

Wazazi wakumbushwa Jukumu la malezı ya watoto

Wazazi na walezi wametakiwa kuchukua hatua kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na sio jukumu hilo kuachia walimu peke yao.

Pia wametakiwa kuongeza ushirikiano na Walimu kwa kufuatilia mienendo ya watoto ili kusaidia watoto hao kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao ya ufaulu.

Hayo yalisemwa na Mwasisi wa Shule ya Sekondari Huria ya Ukonga Skillful, Diodorus Tabaro wakati wa mahafali ya 15 ya kidato cha tano na sita kwa mwaka mmoja, Aprili 30, 2022.

Tabaro amesema wazazi wanastahili kuchukua majukumu yao na sio kuyakimbia. "Kupitia wanafunzi wanaowasajili katika shule yetu tunaona namna ya wazazi wanavyokwepa majukumu yao kwa kutowafatilia wanafunzi wanapokuwa shuleni na hata kushindwa kujua maendeleo ya watoto," alisema Tabaro.

Alisema wanafunzi hao wasipofuatilia kwa umakini wanakuwa wanajihusisha katika makundi mbalimbali yakiwemo kuingia makundi mabaya.

"Changamoto kubwa wanayokumbana nayo wanafunzi ni matatizo ya kitabia ikiwemo makundi rika ambapo zinawafanya kuwa na tabia nyemelezi ambazo kwa asilimia kubwa ndio zilizowafanya awali wengine kutofaulu mitihani yao," alisema.

Alisema miongoni mwa tabia nyingine mbaya ni pamoja na wanafunzi kujihusisha na vitendo vya mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni.

"Kwa shule yetu imekuwa ikijitahidi kwa kiasi kikubwa kuwasoma wanafunzi wetu, na kujua namna ya kutoa suluhu ya matatizo yao kwa kuwapangia vipindi vya ushauri," alisema.

Tabaro alisema miongoni mwa changamoto wanayokumbana nayo ni pamoja na ulipaji wa ada kwa wazazi au walezi kusuasua.

Kwa upande wake Muhitimu wa Kidato cha tano na sita kwa masomo ya mwaka mmoja katika shule hiyo, Stella Nicholas aliwashukuru walimu wa shule hiyo kwa kuwaandaa vema kipindi cha miaka mmoja.

Chanzo: Majira
 
Inategemea na suala la nidhamu ni la mtoto binafsi jinsi anavyochangamana na wenzake waliomzidi umri na aliowazidi umri
 
Back
Top Bottom