Mtoto mchanga analia sana

Mtoto mchanga analia sana

shangwe shangwe

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
108
Reaction score
24
Ndugu zangu naomba ushauri, mtoto wangu anawiki moja tangu azaliwe,analia kwanguvu mara kwa mara. Akisha lia tu,hujisaidia haja kubwa. Pia hutikiswa mara kwa mara(hustuka). Nisaidieni kwa ushauri.
 
Mpeleke hospitali kwa wataalamu kwa uhakika zaidi. Watoto wadogo huwa hawatabiriki. Mchunguze pia kama ananyonya vizuri ili ujue jinsi ya kumuelezea daktari. Mtoto wa wiki moja kujisaidia mara kwa mara ni kawaida, lakini mpeleke kwanza hospitali
 
Ndugu zangu naomba ushauri, mtoto wangu anawiki moja tangu azaliwe,analia kwanguvu mara kwa mara. Akisha lia tu,hujisaidia haja kubwa. Pia hutikiswa mara kwa mara(hustuka). Nisaidieni kwa ushauri.

kwa wiki ya kwanza ndivyo inavyokuwa...tumbo huwa linawasumbua baada ya kuanza kunyonya coz they are not used to.huko kushtuka ni kawaida pia waweza.google,wangu pia alinisumbua ivyo2! kwa uhakika muone daktar
 
Kulia ni kutokana na gas inamsumbua tumboni,anapojisaidia anapata ahueni,kuhusu kushtuka ni mchango dada angu huo,tena kama ni wa kiume hua wanasumbua sana,tafuta wazee wa kabila lako watakusaidia dawa za kiasili,pole sana.
 
Kwa kuongeza tu, jaribu kumuweka mtoto kifuani baada ya kumaliza kumnyonyesha halafu umpapase papase (burp) mgongoni mpaka abehue, hii inasaidia kutoa hewa ya ziada iliyoingia wakati wa kunyonya. Njia hii inasaidia sana kuondoka hiyo gas, fanya hivyo na usiache kwenda kuwaona wataalam kwa ushauri bora zaidi.
Kila la heri kwenye malezi ya kichanga chako.
 
mtoto kulia ni kawaida,maana hiyo ni njia yake pekee ya ku communicate na wewe.kama shejele alivyosema ukishamnyonyesha ,umbebe kichwa kiegemee bega na umpapase mgongoni mpaka ata burp,hiyo inasaidia kupunguza gesi tumboni.
 
kuna dawa inaitwa grip water inasaidia kuondoa gesi kwa watoto,kuanzia watoto wachanga.ukiiona ni kama maji tu
 
Kulia ni kawaida na haja pia .. tumbo huwasumbua sana watt wachanga..epuka kumlazia tumbo kwa ushauri zaidi.
 
Wasije wakawa wachawi wanamustua stua!! Mtafte Mzizi makavu,
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu naomba ushauri, mtoto wangu anawiki moja tangu azaliwe,analia kwanguvu mara kwa mara. Akisha lia tu,hujisaidia haja kubwa. Pia hutikiswa mara kwa mara(hustuka). Nisaidieni kwa ushauri.

Rafiki yangu, kila mmoja atatoa utalaamu wake hapa lakini yote hayo huenda yakatofautiana na mtoto wako. Kama upo Dar, nenda hapa Morocco kuna clinic inaitwa FURAHA MEDICAL CONSULTANT CLINIC, maarufu kwa Dr. Massawe. Rafiki yangu mmoja alikuwa na tatizo hilo hilo na tukamuelekeza huko na mtoto analala usingizi vzr tu.
 
hahahaaaa...!!!. mwanao wa kwanza huyo, utakomaje? halafu huwa wanalia usiku wa manane. mpe mafuta ya samaki halafu uwe unampaka mafuta ya nyonyo kidogo. huwa wanauza madukani. usije sema nyonyo ya mama yake. watoto huwa wanalia hadi wazazi mnalia chezea mtoto wewe. nipe stori mnavyo pokezana na mkeo..hahahaaa...!!!. mara utaambiwa mtafutie jina la kilugha. hapo mama yake hajaanza kulalamika tumbo kuuma hadi apewe safari moja ya moto. lakini usihofu, hayo yataisha tu. kama vipi mcheck doctor. mia
 
1. Mtoto hawezi kulia kama kila kitu kiko sawa. Ukiona analia jua kuwa kuna kitu hakiko sawa. Kama kitu hicho umeshindwa kukigundua na kukitatua basi tafuta ushauri/msaada wa kitaalam.

2. Mama anapoelezea kuwa mtoto wake ana tabia tofauti ni LAZIMA ichukuliwe serious unless proven otherwise. Siungi mkono ushauri wa kutumia google au kuchukulia kuwa ni hali ya kawaida. Gharama yake ni kubwa mno iwapo the guess kuwa ni kitu cha kawaida itakuwa wrong.
 
Ndugu zangu naomba ushauri, mtoto wangu anawiki moja tangu azaliwe,analia kwanguvu mara kwa mara. Akisha lia tu,hujisaidia haja kubwa. Pia hutikiswa mara kwa mara(hustuka). Nisaidieni kwa ushauri.

haja ndo inamuumiza. hata wewe haja yako ikiwa ngumu utajikaza tu vinginevyo ungelia. tatizo la grip water na mafuta ya samaki huwa sometimes yanamletea upele kama yakimkataa. mia
 
Kulia ni kawaida na haja pia .. tumbo huwasumbua sana watt wachanga..epuka kumlazia tumbo kwa ushauri zaidi.
Hapa natofautiana na wewe kumlaza kwa tumbo inampa nafuu zaidi.Pia utakapomuweka begani muweke kwa muda mrefu hata robo saa ili atoe gesi hata zaidi ya mara moja.
 
Hapa natofautiana na wewe kumlaza kwa tumbo inampa nafuu zaidi.Pia utakapomuweka begani muweke kwa muda mrefu hata robo saa ili atoe gesi hata zaidi ya mara moja.
Sikubaliani naww hata kidogo kuhusu kumlazia tumbo. Hata mimi watt wangu nilizoea hivyo! ila nilipokuja kuzalia kwa wenzetu baada ya kutoka hospital unapewa ushauri na masharti... kubwa ni hilo la kutokumlazia mtoto tumbo.
Husababisha matatizo ya moyo na digestion inakuwa si nzuri kwa mtoto. Pia usimlazie ktk mto.
 
Scotts mil 5 asubuhi na jioni.Kuhusu kustuka ni night terrors.Kama we ni mkristu msimulie Bible Stories before bed time.
 
Back
Top Bottom