- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimeona hii huko X
Je, inawezekana mtoto akazaliwa na Malaria?
Je, inawezekana mtoto akazaliwa na Malaria?
- Tunachokijua
- Kwa watoto kuna aina mbili za maambukizi ya Malaria ambapo moja huwa ni maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla au wakati wa kujifungua (Congenital malaria).
Aina ya pili ni Malaria ( ambayo mtoto anaipata baada ya kung'atwa na mbu moja kwa moja.
Kwa mujibu wa case report ya Bugvi na Ahmed inaeleza kuwa;
Malaria ya kuzaliwa (Congenital malaria) ni uwepo wa vimelea vya malaria katika damu ya mtoto mchanga. Ugonjwa huu hupatikana kutoka kwa mama ama wakati wa ujauzito au kipindi cha karibu na kujifungua (wakati wa kuzaliwa).
Katika maeneo yenye maambukizi ya malaria kwa kiwango cha juu (endemic areas), malaria ya kuzaliwa inaweza kujitokeza bila kuwepo historia ya wazi ya homa au uwepo wa vimelea vya malaria (parasitaemia) kwa mama au kwa mtoto wake.
Ikumbukwe kuwa aina zote hizi mbili za Malaria kwa mtoto zinaweza kuhatarisha maisha ya mtoto.
Malaria ya kuzaliwa huweza kupelekea magonjwa na vifo kwa watoto wachanga. Dalili na ishara za malaria ya kuzaliwa si maalum, na zinaweza kuchanganywa na ugonjwa wa maambukizi makali ya damu kwa mtoto mchanga.