Mtoto mchanga kitovu kutoa damu

Mtoto mchanga kitovu kutoa damu

muhuwesichimalamyasi

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
306
Reaction score
132
Wanajf polen na majukumu ya sikukuu.

Waungwana nina mtoto wangu ana siku kumi,tatizo linalomsumbua kitovu chake kinatoa damu.Nimekwenda hospital Dr ameniambia niendelee kukiosha tu bila kunipa dawa.

Naomba mwenye kufahamu dawa au ushauri aniambie.
 
Pole sana. Watoto wachanga wengi huzaliwa na upungufu wa vitamini K na hivyo kusababisha damu kushindwa kuganda. Hii hupelekea damu kuendelea kuvuja sehemu iliyo na mchubuko au ilipochomwa sindano au kwenye kitovu wakati bado hakijakauka vizuri. Ndo maana kuzuia hii hali watoto wote wachanga inashauriwa wachomwe sindano ya vitamini K mara tu baada ya kuzaliwa. Kwetu Tanzania hili halifanyiki hasa kwa hospital za pembezeno kutokana na kutokakujua lakini pia mara nyingi hukosekana hospitali japo pharmacy hizi vitamini k zipo kwa wingi. Hali hii hupelekea watoto wengi wachanga kufa kwa kupoteza damu.

Hivyo nakushauri mwanao mpeleke haraka kwa daktari wa watoto ili amchunguze na kumpa vitamini K. Kama huwezi kumuona daktari wa watoto waweza nunua vitamini k pharmacy na kwenda nayo hospital ya karibu ili wamchome. Tafadhali usimchome mwenyewe.
 
Mpeleke kwa dr mwingine wa watoto. Hofu kubwa ni kupata infection.

Kila la kheri
 
pole sana. Mimi iliwahi kunitokea wakati mwanangu ana siku 12. Dr. alinishauri nikimaliza kumuogesha nimpake spirit then nipafute baada ya muda mfupi pabaki pakavu wakati huohuo nizuie infection. Pia alinishauri nisimvalishe nguo mapema maana nilikuwa na kiherehere cha kimvalisha mtoto magauni. Aliniambia nguo zinapomgusa pale zinamtonesha maana kinakuwa hakijapona vizuri bado. Tumia tu dawa ulizopewa na dr. na ukiepushe na infection pia uwe makini na mavazi ya mtoto katika umri huo. Kikiwa na dalili za usaha mkimbize haraka hospital. Malezi mema
 
ahsante ni kwa ushauri wenu wana jf,kesho nitakwenda hospital kuuliza km alichomwa sindano ya vitamin k.na kwa kuanzia Leo nitampaka spirit.
 
Back
Top Bottom