TANZIA Mtoto mchanga wa Marehemu Mbunge Irene Ndyamkama afariki dunia

TANZIA Mtoto mchanga wa Marehemu Mbunge Irene Ndyamkama afariki dunia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FRppZSxWYAEHcJk.jpg
Mtoto mchanga aliyeachwa na marehemu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama amefariki dunia jana Aprili 30, 2022.

Mtoto huyo amefariki baada ya kuishi kwa siku saba tangu kuzaliwa kwake, Mbunge Irene alifariki dunia Aprili 24, 2022, katika Hospitali ya Tumbi wakati akipatiwa matibabu baada ya kujifungua mtoto huyo.

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Irene Alex Ndyamkama yaliyofanyika Aprili 29, 2022, Nsimbo Mkoani Katavi

Source: East Africa TV
 
Mtoto mchanga aliyeachwa na marehemu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama amefariki dunia jana Aprili 30, 2022.

Mtoto huyo amefariki baada ya kuishi kwa siku saba tangu kuzaliwa kwake, Mbunge Irene alifariki dunia Aprili 24, 2022, katika Hospitali ya Tumbi wakati akipatiwa matibabu baada ya kujifungua mtoto huyo.

Source: East Africa TV
Pole kwa familia ya mbunge
 
Baada ya Mama kuitwa, akaogopa kuhusu maisha ya kachanga chake, katalelewa na nani?. Akaogopa katateseka akaamua kukaita na kwenda nacho kichanga chake.

Najua wengi hawalijui hili

Naamini family itakalaza kachanga halo, ubavuni kwa mama yake alipolazwa.
Rip Mbunge, Mama na Mwana

P
 
Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Baada ya Mama kuitwa, akaogopa kuhusu maisha ya kachanga chake, katalelewa na nani?. Akaogopa katateseka akaamua kukaita na kwenda nacho kichanga chake.
Najua wengi hawalijui hili

Naamini family itakalaza ubavuni kwa mama yake alipolazwa.
Rip Mbunge, Mama na Mwana

P
Acha fix mkuu hakunaga manjangunjangu ya namna hii! Huwa ni fahari kwa mzazi kuacha mtoto duniani kwani huyo mtoto hakuwa na baba mpaka akose wa kumlea..?
Ipi nafasi ya baba kama ameitwa na mama..?
Kwahiyo baba hakuwa na nafasi ya kukaa na mwana isipokuwa mwana lazima aende na mama tu!

Hivi vitu vyengine sijui huwa mnavitolea wapi!,acheni nature ifanye kazi yake kama kuna makosa yalifanyika ktk maswala ya afya basi na yafanyiwe kazi.
 
Inauma saana, Daaah!!

Nimeandika na kufuta huku nimejishika tama!

Niseme tuu Kwa ujumla, Serikali inawajibu wa kuboresha huduma za afya, na tunaowapa madaraka kutuongoza wawe wakali kila wasikiopo mmoja wa wateule wao amefuja pesa, akamatwe na arudishe pesa ili zikaboreshe huduma vijijini
 
CCM tunaomba mjifunze kuhusu sekta ya afya kama ilivompata mwenzenu kuwa sisi msio tujali basi tunaumia kama nyie mlivoumia
 
Baada ya Mama kuitwa, akaogopa kuhusu maisha ya kachanga chake, katalelewa na nani?. Akaogopa katateseka akaamua kukaita na kwenda nacho kichanga chake.
Najua wengi hawalijui hili

Naamini family itakalaza kachanga halo, ubavuni kwa mama yake alipolazwa.
Rip Mbunge, Mama na Mwana

P
Japo nakubaliana na ww mambo mengi Ila hapo BIG NO
 
Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, nazo zimejaa tabu na shida.

Bwana alitoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe...Ameen.
 
Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, nazo zimejaa tabu na shida.

Bwana alitoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe...Ameen.
kwani kuna binaadam wengn huzaliwa na asiekua mwanamke?
 
Back
Top Bottom