sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ilikuwa ni tarehe 21-11-2020 siku ya Jumamos ambapo mtoto Nassir Jumanne mande mwangopola alipotea Chunya mjini, moja ya wilaya ya Mbeya.
Wazazi wa mtoto, baba yake Jumanne Mwangopola na mama yake Shamimu Shabani walifanya jitihada kubwa kumtafuta lakini jitihada hazikuzaa matunda.
Leo hii kupitia group maarufu la facebook la Mbeya, kuna mdau aliifowadi post ambayo aliiona kwa mtu anaeishi maeneo ya Tunduma mitaa ya Majengo, aliweka post kwamba kuna mtoto aliwahi kuja karibu na sehemu anayoishi na alikuwa harusiwi kutoka, ni mpaka hivi karibuni ndio alianza kuruhusiwa kutoka na akagundua ni mtoto anaetafutwa.
Kwa bahati nzuri wazazi wa mtoto ni wanachama wa hiki kikundi na walipoiona hio post kwa wakapeana mawasiliano na mtu aliefowadi,
Kuhusu kilichoendelea mpaka sasa hakijulikani ila huenda siku za karibuni tukajua