SoC02 Mtoto ndani ya giza jeusi

SoC02 Mtoto ndani ya giza jeusi

Stories of Change - 2022 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
MTOTO NDANI YA GIZA JEUSI.

Mimi ndio taifa la kesho kweli kwa haya uliyonitendea?


Nikifiwa na wazazi wangu sina amani tena ya kesho, wazazi wakinipeleka shule za hosteli nikiwa bado mdogo sina raha kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji ninavyofanyiwa na kaka zangu, nikiwa nyumbani na babu yangu naogopa kunajisiwa, nikiishi kwa baba yangu mkubwa naogopa kwani sitoenda shule kwa kupewa kazi ya kuchunga ng’ombe mbugani, nilidhani dada zangu tu waweza kufanyiwa hivyo kumbe mimi ndio zaidi kwani naharibiwa njia yangu ya haja kubwa, ee Mwenyezi Mungu tumaini la kesho yangu lipo kwako tu.

Kwanini unitendee haya! Kweli unanilawiti, unaninajisi, mbona nyie hamkufanyiwa haya? Ona nimetolewa bikra kabla ya wakati wangu, ona haja yangu kubwa inavyotoka yenyewe! Ona nilivyokonda kwa sababu ya maradhi uliyoniambukiza, hata shule siwezi kwenda tena kwa amani! Jamani mimi…. ee Mwenyezi Mungu nifanyie wepesi katika taabu zangu hizi

Najua unanishangaa kwa sababu ya mwonekano wangu, ona mwili wangu ulivyojaa makovu, madonda kila sehemu, wakati mwingine namwagiwa maji ya moto, na mara nyingine nachomwa na vijinga vya moto kwenye mwili wangu na hata kuingiziwa vijinga hivyo sehemu zangu za siri na mara nyingi tu njia yangu ya haja kubwa, kwa sasa ninanuka, kwa kujikojolea na kujinyea sijapenda ila kwa sababu yako wewe kaka yangu, wa sababu yako wewe baba yangu, kwa sababu yako wewe babu yangu, kwa sababu yako wewe nimekuwa hivi, nilikuamini wakati naenda shule kwamba unaniwahisha kwa pikipiki yako ili nikapige namba ila wewe ukanipeleka kichakani kuniharibu ukanifanya hivi! Niliona wewe ndio faraja yangu baada ya wazazi wangu kufariki ila nawe umekuwa sababu ya maumivu yangu, nilikuamini kwamba wewe utanilea baada ya kufiwa na wazazi wangu ila wewe ukanifanya mkeo, sasa ona umri wangu miaka saba hata nisingeweza kukupikia ila sasa umeniachia maradhi yako yaliyomuua bibi yangu! Hata kesho yangu siioni badala ya kaburi ninalolichungulia!!!

Jana nilikuona shangazi yangu, uliingia chumbani kwangu na nilikusalimia hukuitika lakini uliniona, baadaye mliingia tena mkiwa na baba yangu mkubwa nikawasalimia tena hamkuitika ila mliniona najua hamkuwapenda wazazi wangu ila mimi sikuwepo kipindi cha uhai wao, nimesikia mengi kwamba alishindwa kuwasomesha wakati alikuwa na mali, kwamba hakuwatunza vema wazazi wake ila mimi sikuwepo, kwamba hata wadogo zake hakuwasomesha ila mimi sikuwepo! Adhabu niliyoipata yatosha kitandani kwangu ni maumivu kwani najikojolea muda wote, najinyea muda wote kwa adhabu niliyoipata ya kuondokewa na wazazi na nyie mkashindwa kunilinda.

Natamani anione Shekhe, anione Padre, anione Mchungaji, anione muungwana yeyote, anione mtu mwenye hatima ya maisha yangu ili akauambie umma machungu ninayo yapitia, mtu atakayefanya upya hatma ya maisha yangu ili nifanane na watoto wengine. Najua wengi wamepata habari zangu ila hawakuweza kuongea, najua wapo wenye uchungu na maumivu yangu ila wanaogopa kuongea, ni nini shida ya kuwambia watu wema maumivu ninayo yapitia mimi? Au ni mali walizonazo ndugu zangu? Mnaogopa uchawi wa babu?

Muda mwingi nawaza nani atakayeniokoa katika maumivu haya? Muda mwingi wanaoniona ni wale wasio na msaada kwangu na wenye msaada na maisha yangu hawanioni kwa sababu nimefichwa ndani ya nyumba hii, najiuliza hii nyumba ndio kaburi langu? Najua na wewe unatamani nipumzike kutoka kwenye dimbwi la maumivu haya lakini hunioni japo sipo mbali na wewe, tafadhali nitafute nimefichwa ndani ya nyumba ambayo maovu mengi ndimo natendewa, ee mwenyezi ondoa upofu kwa waungwana hawa ili wafumbue macho yao na kunipa msaada wa hatma ya maisha yangu.

Najua unajiuliza wawezaje kutoa habari zangu mimi, nikushauri tu wala usiogope, paza sauti yako ili nipone au nawashauri muandike kwenye karatasi na mkadondoshee kwenye sanduku la maoni ya mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kijiji au wa kata mkiweza zaidi pelekeni kikaratasi hicho kwenye sanduku la maoni ya Mkuu wa wilaya ili nisaidiwe kama mtaweza zaidi basi mkawaambie dawati la jinsia na watoto katika vituo vyote vya Polisi au kwa Maafisa wa ustawi wa jamii walioko katika nchi nzima.

Wewe pekee ndio mtu wa kuokoa maisha yangu na kutengeneza kesho yangu, ukinifichua mimi ujue ya kwamba umemulika uovu wanaofanyiwa watu kama mimi ndani ya jamii yetu, utakuwa umewamulika wote wanaotekeleza vitendo vya ukatili kwa watoto wote ndani ya jamii yetu, utakuwa umeweka msingi mzuri kwa kesho ya watoto wote wenye maisha magumu, walemavu, yatima, na wote wanaohtaji msaada kama wangu mimi.

Nakuombea kwa mwenyezi Mungu akulinde dhidi waovu wote ambao hawapendi kutuona na sisi tukiwa na furaha, kwani kwa kunisaidia mimi na wenzangu ambao tumefichwa majumbani umelisaidia taifa kupata wasomi ambao walikuwa hawana ndoto ya kufikia walipo, umesaidia walemavu kupata elimu, umesaidia yatima kupata elimu, umewasaidia wote kuwatengenezea kesho yao, na umelisaidia taifa kupata viongozi kutoka makundi yote zaidi sana kundi letu la wasiojiweza baada ya kukumbana na maswahibu ya walimwengu wa dunia hii. Sasa naona kesho yangu iking’ara kama jua, kama nyota na najona nikiwa kiongozi nitakaye wapazia watoto wengine sauti dhidi ya maovu wanayoweza kufanyiwa na dunia hii na yote haya nayaona yakifanikiwa kwa sababu yako wewe ambaye ameamua kuyafanyia kazi maombi yangu haya, ninakuombea kwa mwenyezi Mungu akubariki na akufanye kuwa Baraka kwa wote. Kwa maombi haya naamini utapaza sauti na kuzidi kufichua watoto wote wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ili kufikia ndoto na malengo yao. AMEN.
 
Upvote 4
Uko vizur kura yangu umepata na ww kasome langu.
 
Back
Top Bottom