Rayan: Mvulana wa Morocco aliyetumbukia kisimani afariki
Saa 3 zilizopita
CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Wazazi wa Rayan wakiondoka eneo la tukio baada ya mwili wa mtoto wao wa kiume kupelekwa kwa ambilansi
Mvulana mwenye umri wa miaka mitano aliyeanguka kwenye kisima kirefu kwa siku nne amefariki, licha ya juhudi za kumuokoa.
Taarifa ya ufalme wa Morocco ilitangaza kifo mara ya baada ya mvulana huyo kuondolewa kwenye shimo.
Juhudi za kumuokoa mvulana huyo, anayeitwa Rayan, zilifuatiliwa kote nchini, huku mamia ya watu wakikusanyika kwenye shimo na maelfu zaidi wakifuatilia shuguli ya uokozi ,kupitia mtandao.
Mvulana huyo alitumbukia katika iisma cha urefu wa mita 32 (futi104) , licha ya kwamba shimo hilo lilikuwa jembamba . Uokoaji ulitatizwa na hofu ya kuporomoka kwa ardhi juu ya shimo hilo.
Hatimaye waokoaji walimeta nje mvulana Jumamosi jioni.
Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu hali yake wakati huo, na uokoaji huo ulishangiliwa na umati wa watu.
Kwenye mitandao ya kijamii, watu walitumia msema wa alama ya leri- hashtag #SaveRayan,ambayo imekuwa ikisambaa kote nchini humo na nje ya mipaka ya nchi hiyo, huku watu wakielezea kufurahishwakuokolewa kwa mvulana huyo.
Lakini iligeuka kuwa dakika za kuvugunja moyo wakati taarifa ilipotangazwa kwamba Rayan alifariki.
Watumiani wa Twitter baadaye walianza kutoa salama zao za rambirambi na kuelezea huzuni kwa kutumia alama sawa ya leri.
"Kufuatia ajali ya mtoto Rayan Oram, Mfalme Mohammed VI aliwaita wazazi wamvulana aliyefariki baada ya kutumbukia ndani ya shimo " taarifa ya kasri ya rais ilisema.
Siku ya Jumamosi, vyombo vya habari viliripoti kwamba waokoaji walikuwa mita 1.8 kutoka alipokuwa mvulana huyo.
"Tumekaribia," mmoja wa viongozi wa operesheni hiyo, Abdesalam Makoudi, alisema Ijumaa mchana.
"Tumekuwa tukifanya kazi bila kukoma kwa siku tatu na uchovu unaanza, lakini timu nzima ya uokoaji bado iko hapa inaendelea na kazi."
Wakiongozwa na Kurugenzi ya Ulinzi wa Raia wa Morocco, shughuli za uokoaji katika mji mdogo wa kaskazini wa Tamorot, karibu kilomita 100 (maili 62) kutoka mji wa Chefchaouen, zilianza tangu Jumanne jioni.
Barabara zinazozunguka mji huo zilijaa magari na mabasi, huku maelfu wakishangilia waokoaji katika eneo la tukio.
CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Watu walikusanyika kutazama shughuli ya kumuokoa kijana hiyo inavyoendelea siku ya Jumamosi
'Sijalala kabisa'
Baba yake Rayan alikuwa akitengeneza kisima wakati wa ajali hiyo inatokea, na alisema yeye na mama yake Rayan walikuwa "wamefadhaika na wenye wasiwasi mwingi."
"Katika muda huo, nilikuwa nimeondoa macho yangu kwake kidogo tu, nahapo ndipo alipoanguka kisimani. Sijafumba hata jicho tangu mwanangu alipotumbukia," aliambia tovuti ya habari ya le360 siku ya Jumatano.
Akiongea na vyombo vya habari vya Morocco huku akibubujikwa na machozi, mama yake Rayan alisema: "Familia nzima ilitoka kumtafuta. Kisha tukagundua kuwa alikuwa ameanguka chini ya kisima. Bado nina matumaini kwamba tutampata akiwa hai."
Picha za Alhamisi kutoka kwa kamera iliyoshushwa kisimani zilionyesha kuwa mvulana huyo alikuwa hai na ana fahamu, ingawa alionekana kuwa na majeraha madogo kichwani.
Wafanyakazi wa uokoaji wameshusha barakoa ya oksijeni, chakula na maji ndani ya kisima na timu ya matibabu pia iko kwenye eneo la tukio, tayari kumtibu mvulana huyo.
Helikopta pia imefika eneo la tukio ili kumpeleka hospitali mara baada ya kutolewa kutoka kisimani.
......
SIJUI INGEKUWAJE HAPA NYUMBANI KWETU NAONA NI KAMA KABURI LINGEWEKWA KWA JUU TU..