Mtoto sio wake

Mtoto sio wake

PRECIOUSDOE

Senior Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
114
Reaction score
12
Wana jamii,

Ndugu yangu amekuwa akimlea mtoto msichana aliye fikiri ni wake ,mtoto anaishi na nyanya yake lakini ndugu yangu humtembelea mara kwa mara na humlipia fees, medical na mambo mengine financial support.Juzi akaelezwa kwamba mama ya yule mtoto amewambia wanaume wengine watatu eti mtoto ni wao ndio apata uhisani wa kifedha kutoka kwao.Ndugu yangu alikuwa anasema mtoto huyu ana fanana naye lakini since aipate habari hii hataki kumwona mtoto yule au kusikia lolote kumhusu.Juzi akaniambia yakwamba hata mtoto akilazwa hospitalini yeye hawezi akamtembelea.Mimi nika mwambia afanye DNA kabla ya ku fanya uamuzi wowote because huenda akawa mtoto niwake.Mamake mtoto alikuwa bikira walipokutana na ndugu yangu lakini after that akaingia kwenye maisha ya raha na kwa sasa hivi anayaishi maisha ya ukahaba na ulevi hadi hana wakati wa kumshugulikia ule mtoto.Tafadhali nipe mawaidha on what is the best way to handle this.Ndugu yangu amevunjika moyo kwa sababu alikuwa anampenda sana yule mtoto.
 
Poleni sana. Amchukue mtoto wakafanye vipimo. Baada ya vipimo uanzishe thread la feedback tukushauri cha kufanya.
 
anachohitaji ni kupima tu. atulize hasira, akapime! Anaweza akamtelekeza mwanaye................
 
la maana ni vipimo tu hapo ili ajue kama mtoto ni wake hama la
 
Hayo ndiyo madhara ya kufanywa fanywa hovyo hovyo kama kuku. Ni yamkini hajui hata baba wa kweli ni yupi. Pia inawezekana anajua lakini kwa ulafi wake anaona poa kuchanganya watu akili.

Ni mbaya sana kulea mtoto ambaye unadhani ni wako kumbe ukweli wa mambo si wako. Oh wait...nilisahau....wanawake ni wema sana na hawawezi kufanya kitu kama hicho. Jamaa kachanganyikiwa tu.
 
Ushauri wako ni mzuri sana, apime maana huyo mlevi na kahaba huwezi kuamini maneno yake.
 
Mbona hapo kuna kaukweli kuwa huyo mama anataka pesa tu, uwezekana wa kuwa mtoto ni wake utathibitika pale DNA check up itakapohusishwa, asiyaamini sana maneno ya huyo mama kwani huenda ikawa ni njia moja wapo ya kujipatia kipato kutoka kwa hao wajameni. Aendelee kumpenda mtoto na hata kama akithibitisha kuwa sio wake yeye asiache kumpenda kwani huyo ni malaika tu hana makosa.
 
Hayo ndiyo madhara ya kufanywa fanywa hovyo hovyo kama kuku. Ni yamkini hajui hata baba wa kweli ni yupi. Pia inawezekana anajua lakini kwa ulafi wake anaona poa kuchanganya watu akili.

Ni mbaya sana kulea mtoto ambaye unadhani ni wako kumbe ukweli wa mambo si wako. Oh wait...nilisahau....wanawake ni wema sana na hawawezi kufanya kitu kama hicho. Jamaa kachanganyikiwa tu.

Some advise....:sick:
 
Some advise....:sick:

The lady should just come clean and fess up. Why lie about your own child? To me that is complete and utter foolishness. She should just fess up and deal with the aftermath like a grown woman that she thinks she is because lying ain't gonna get her anywhere.
 
Nyani, nafikiri unakuwa mkali sana then hutoi ushauri, hapa mdada anaomba ushauri wa kumsaidia huyu ndugu... tatizo limeshatokea, hasomi messages za JF, so hata ukisema vp hapati ujumbe... Mshauri jamaa aachane na huyo mtoto au akapime DNA
Ubarikiwe sana
 
Dada Askofu, nadhani unanisoma vibaya. Sawa, tatizo limeshatokea. Sasa ili kuondoa utata njia pekee iliyobaki ni kwenda kupimwa damu tu. Na hili wala mtu huhitaji ushauri kwa kweli labda uniambie huyo mdada/ mkaka hajui kuhusu uwepo wa uwezekano huo.
 
Asikate tamaa yawezekana mtoto wa kwake kweli asiyasikilze maneno ya mama yake na mtoto kwani yupo kimaslahi zaidi na inawezekana kuwa anawadanganya hao wanaume wengine ali apewe hela na kumtunza mtoto cha msingi hapo ni kupima DNA asije mtelekeza mtoto wake kisa maneno ya watu
 
Dada Askofu, nadhani unanisoma vibaya. Sawa, tatizo limeshatokea. Sasa ili kuondoa utata njia pekee iliyobaki ni kwenda kupimwa damu tu. Na hili wala mtu huhitaji ushauri kwa kweli labda uniambie huyo mdada/ mkaka hajui kuhusu uwepo wa uwezekano huo.

Miafrika Ndivyo Tulivyo.
 
Kisheria...........mama wa mtoto akisha mtaja mwanamme kuwa ni baba basi sheria inamtambua mwanamume huyo kama baba wa mtoto huyo,utetezi pekee alionao ni kuihakikishia mahakama kuwa hakuwahi kutembea(kufanya ngono) na huyo mwanamke, lakini kwa wakati huu ushahidi wa DNA unaweza kutumika katika ku disprove that fact,

.....Lakini kama watu wanaweza ku adopt watoto wa watu hata wasiowajua na kuwafanya wa kwao kisheria???? kuna ubaya gani ndugu yako akimchukua tu huyo mtoto na kuendelea kumlea kama wake??(kama kweli alimtoa bikira=kitanda hakizai haramu)

Ndugu yako analo.................................alibebe.
 
Wala asipime DNA,amlee tu huyo mtoto akiamini kuwa ni wake. Jins huyo mama asivyoeleweka ndugu yako akimtelekeza huyo mtoto ataishi maisha magumu sana.
 
Mshauri aendelee kumlea mtoto hata kama si wake for the sake of that child. Siku zote mtoto amekuwa akijua nduguyo ndiye babae sasa akimkana atamuumiza kisaikolojia maisha yake yote.
 
Mshauri huyo ndugu yako asichukue uamuzi wa haraka kumtelekeza mtoto. Huyo mama wa mtoto ameshaonekana mapepe. Pengne pombe tu zinamuongelesha. Akapime DNA kwisha kazi.
 
Back
Top Bottom