Mtoto wa Aunty azua zengwe, hafanani na Moze Iyobo

Mtoto wa Aunty azua zengwe, hafanani na Moze Iyobo

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mtoto wa kike wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson aliyejifungua mwishoni mwa wiki iliyopita na kumpa jina la Cookie (keki ndogo lakini tamu) anaanza kung' aa kwenye vyombo vya habari baada ya baadhi ya watu kumpiga zengwe la madai kwamba eti hafanani na baba yake .

Huku ishu hiyo ikipingwa vikali na Aunt , washakunaku wa mambo ya watu waliozungumza na Amani baada ya kumuona Cookie walidai kwamba mtoto ni mweupe wakati Moze ni mweusi ' tiii' .Zengwe hilo lilianza kusambaa miongoni mwa mashosti waliokwenda kumpa hongera Aunt nyumbani kwake , Kinondoni, Dar , saa chache baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini .

"Unajua tangu akiwa mjamzito kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona mtoto kujua kama kweli ni wa Moze maana mwanzoni hakuna aliyeamini kama mimba ni ya Moze ' so' hao ndiyo wameanza chokochoko , " kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutochorwa gazetini .

Baada ya kunasa zengwe hilo , Amani lilimtafuta Aunt ili azungumzie ishu hiyo ambapo alifunguka;

Amani : Kuna zengwe juu ya baba wa mtoto wako , kwani mwanao anaitwa nani ?

Aunt: Anaitwa Cookie Lapri - Center .

Amani : Yaani Lapri - Center ndiyo jina la ukoo?

Aunt: Mambo mengine hayawahusu . Mnataka jina la ukoo la nini ?

Amani : Watu wanauliza, wanataka kujua maana tayari kuna zengwe juu ya baba wa mtoto .

Aunt: Acheni mambo yenu (kisha akakata simu ).

Aidha , madai kutoka kwa chanzo chetu ni kwamba baada ya kuibuka kwa zengwe hilo , Aunt ameamua kumficha mtoto wake .

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • 1432812756482.jpg
    1432812756482.jpg
    15.2 KB · Views: 3,669
Sasa anamfichia nn? Anataka kujifanya na yeye nini blue ivy?
 
Hili jina la mtoto kiboko aisee loh cookie la pri ........... Labda huo weupe na wa kitoto tu akikua atabadilika.
 
jina la baba ndo hilo lapri kwanza ni nini maana ake na ikiwa baba anaitwa mose iyobo imekuaje aitwe cookie lapri ha ha ha h a ni shida aseee
 
jina la baba ndo hilo lapri kwanza ni nini maana ake na ikiwa baba anaitwa mose iyobo imekuaje aitwe cookie lapri ha ha ha h a ni shida aseee

Mwenzangu mmh kazi ipo mwka huu, loh mpaka tumjue baba watoto sisi ndo wambea wa mujini
 
ahahaha utasubiri sana mmbea mwenzangu

UMbea utanishinda huyu aunty anataka kutuzid akili eeh, ngoja ivi kajifungulia hospital gan? Nataka nikamhonge dokta aniambie kadi jina la baba kaandika nani, maana madokta kwa umbea na kutoa siri za watu hajambo
 
Kwani alijifungulia wap jaman nikapeleleze nipate kujua kadi mtoto kaandikwa nani, haiwezekan iasehh

Mwenzangu hata sijui ni hospital gani kajifungulia mweeeh. Mama cookie la pri center noooma. May be mbuga zetu ndo baba wa mwana.
 
Kwani alijifungulia wap jaman nikapeleleze nipate kujua kadi mtoto kaandikwa nani, haiwezekan iasehh

Hahahahahaa binamu umbea huu utakufanya umwagiwe tindikali, shauri zako.
 
Moze ukute ni baba mlezi tu mtoto wa Jemba lingine huko loh!

Na ngoja tutaona tu.Kwani mtoto akikua si atapigwa picha? Yule iyobo ana mtoto aliyezaa na mwengi ni copy ya iyobo wala huulizi.
Labda anasubiri 40 ipite ndio atuoneshe mtoto.
 
sijui hozpitali gani huko Mbezi beach
kama baba sio Iyobo basi atakuwa yule waziri wa utalii

Kama mbezi itakuwa massana tu, ntaenda kuongea na dokta lema anipe file la aunty aiseeh, maana na umbea huu ata mpaka nimjue baba watoto,maana umbea ndo kaz yangu
 
Back
Top Bottom