GE2025 Mtoto wa Celina Kombani apeta Kura za maoni

GE2025 Mtoto wa Celina Kombani apeta Kura za maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mtoto wa Celina Kombani, Lucy na Mkurugenzi wa zamani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Sheila Lukuba wameibuka kidedea katika kura za maoni za Jumuiya ya Wanawake UWT Mkoa wa Morogoro baada ya kupata kura 1,314 na 597 mtawalia.

Screenshot 2025-07-31 084824.png
Lucy Kombani na Sheila waliwagaragaza wagombea wengine saba kusonga mbele katika safari ya kuwa wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro.

Matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Jumatano yameonesha ⁠Josephine Kapoma amepata kura 454, ⁠Mwandishi wa habari na mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Jane Mihanji (kura 339), ⁠Mfanyabiashara Aliyah Awadhi Omary (236), Mtumishi wa BoT, ⁠Amina Karuma (153), ⁠Mwalimu Hajira Mwikoki (kura 90), Mtumishi wa COSTECH, ⁠ Dk. Kulwa Kangeta (75), na ⁠Mtoto wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa mbalimbali nchini Stephen Mashishanga, Bi Rachel Mashishanga akipata kura 35.
 
Tanzania ilikuwa Jamhuri na kukataa vyeo vya kurithishana, ila kwa sasa tumerudisha uchifu kwa aina tofauti tu.

Kila mtoto wa mbunge anataka kuwa mbunge.
Ndio sehemu pekee kipato kizuri, mali zako zinakuwa salama na deals zako nyingine haramu ni mwendo wa kupiga simu tu.
 
Back
Top Bottom