Mtoto wa Charles Kimei afunga ndoa Jijini Dar. Kweli mjini pesa shikamoo kelele

Good for them....

By the way harusi/sherehe ya harusi kwa pesa waliyonayo ingelipendeza kama ingefanyika mandhari fulani ya ufukweni au sehemu ya wazi nje na mida ambayo jua halijakuchwa/halijachwea...

Hizi za usiku huwa vurugu vurugu na walevi ndio hujaa sana huko...
 
Ndoa maaskofu watatu. Hivi na za waumini wa kawaida huwa zinakuwa hivi? KKKT kwa kupenda wenye pesa tu. Yaani Shoo katoka Kilimanjaro kuja kufungisha ndoa Dar?Ama kweli Yesu peke yake ndo hakuwa mbaguzi.

Na mimi limenishangaza hilo kwa kweli. Kumbuka sio maaskofu watatu tu, hapo kuna aliyekuwa top na top mwenyewe wa KKKT. Ph.D holders etc.
 
Ndoa maaskofu watatu. Hivi na za waumini wa kawaida huwa zinakuwa hivi? KKKT kwa kupenda wenye pesa tu. Yaani Shoo katoka Kilimanjaro kuja kufungisha ndoa Dar?Ama kweli Yesu peke yake ndo hakuwa mbaguzi.
wewe unajua urafiki uliopo kati ya Kimei na hao viongozi wa dini au ushamba unakusumbua?
 
Ukisikia mambo mengi muda mchache ndio hapo.Hapo watu wanataka kujiachia wakitoa zawadi zao,unaweza ukakuta walio jiandikisha kwa Dj kutoa zawadi wamejaza Counter Book Quire 2.
Hahahah
 
Hivi lini ignorance itaisha miongoni mwetu sisi watanzania? Mwenye hii comment unaonekana una kila dalili ya chuki na ukabila, yeyote anaetukuza ukabila na kufanya justification juu ya hilo hasa kwenye hadhara kama hapa hatufai Kwenye jamii.

Uchapakazi, weledi, juhudi na kiu ya maendeleo haina ukabila,dini, rangi au vyovyote vile, bali hii hutokana na silika, kariba, uthubutu na kujituma kwa mtu mwenyewe, anaweza kuwa unatoka kabila lolote lile, au dini yeyote ile nk. Na pia kinyume chake, wapo wachaga walevi na masikini pia, lakini pia wapo wachaga wavivu, na hii ina kuwa applied kwa makabila, dini, na watu wa aina zote.

Mimi sitetei uvivu wa jamii fulani bali natetea utanzania na uhalisia wa mambo yalivyo. Nakushangaa mtoa post unapodhihaki jamii ya watu wa pwani hasa ukiwalenga wazaramo ( "wacheza mdundiko") kuwa ni wavivu wakti kuna waziri ni mzaliwa wa Uzaramuni kabisa Kwala-Samvula Chole (Jaffo Seleiman) anaongoza wizara yake kwa weledi wa hali ya juu kbs pengine kuliko hata baadhi ya mawaziri wengine wanaotoka bara, au kaskazini nk.

CRDB kuna wachaga wengi, kama watu wanavyodai, Yes, inawezekana kutokana na sababu fln fln, lkn uchaga wao siyo uliowapeleka pale, bali walikidhi vigezo. Mtu wa kundi fln anaenda ngomani, Yes, tumthamini pia, kwani ana play part fln mhm kwenye kutunza na kuthamini mila, desturi na tamaduni zetu. La muhimu zaidi yatupasa kujua ni kuwa, maisha lazima yawe balanced, hatuwezi wote kuwa tunafanana kwa kila kitu.

Hitimisho langu ni kwamba, tuwe na deal na mtu kama mtu juu ya uweledi au udhaifu wake, na siyo kufanya mambo ya ku generalize kuhusisha makabila, nk.

Adios!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…