Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Binti wa mwanamuziki Chris Brown, Royalty Brown mwenye miaka 11 kwa kushirikiana na Influencer wa mitandaoni Zachery Dereniowski ameamua kumzawadia mwanamama mmoja pamoja gari jipya na pesa taslimu dola 10,000 ambazo ni sawa na pesa za Kitanzania milioni 24 kama sehemu ya shukrani.
Kwa mujibu wa Zachery, binti huyo (Royalty)alitaka kuungana nae kutengeneza maudhui ya kipekee na yatakayoacha alama kwa shabiki mmoja wapo wa baba yake (Chris Brown) ndipo wakaenda nje ya ukumbi na kumchangua mama huyo na binti yake wakati wa Tamasha la ‘Breezy Bowl’ huko Detroit, Marekani.