Mtoto wa Freeman Mbowe (Nicole) aachiwa na Jeshi la Polisi

Nicole Mbowe ambaye ni Mtoto wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameachiwa huru na Polisi ikiwa ni zaidi ya saa mbili toka alipokamatwa maeneo ya Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam leo September 23,2024.

- LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Nicole ameonekana nje ya Kituo cha Polisi cha Oysterbay akiwa na Mama yake Mzazi (Mke wa Mbowe), Lilian Mtei pamoja na Wakili Peter Kibatala ambapo hata hivyo hakuweza kufanya mahojiano na Wanahabari kuelezea kilichotokea hadi kuachiliwa kwake.

Mapema leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne katika mkutano na Waandishi wa Habari alipoulizwa kuhusu kushikiliwa kwa Mtoto huyo, alisema hayumo katika orodha ya Watu 14 waliokamatwa leo katika sakata la maandamano ya September 23.

-
Nilichogundua katika hii picha, mke wa mheshimiwa Mbowe ni mashallah, ila sasa sura imeanza kujenga nje ya beacon (upara)
 
TZ bana, Bado tuna la kujifunza hivyo Kila kitu huenda Kwa hatua.
 
Nicole Mbowe ambaye ni Mtoto wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameachiwa huru na Polisi ikiwa ni zaidi ya saa mbili toka alipokamatwa maeneo ya Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam leo September 23,2024.

- LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Nicole ameonekana nje ya Kituo cha Polisi cha Oysterbay akiwa na Mama yake Mzazi (Mke wa Mbowe), Lilian Mtei pamoja na Wakili Peter Kibatala ambapo hata hivyo hakuweza kufanya mahojiano na Wanahabari kuelezea kilichotokea hadi kuachiliwa kwake.

Mapema leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne katika mkutano na Waandishi wa Habari alipoulizwa kuhusu kushikiliwa kwa Mtoto huyo, alisema hayumo katika orodha ya Watu 14 waliokamatwa leo katika sakata la maandamano ya September 23.

-
Ni jambo jema
 
Back
Top Bottom