Mtoto wa kike akiwa ugenini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wengi wetu huwa tunaishi na wazazi na ukitoka kwa wazazi unakwenda boarding school baada ya hapo chuo na kuanza kazi. Hakuna formula moja ya maisha, kwa sababu hii na ile inabidi uishi na ndugu na jamaa kwa muda mfupi au mrefu.

Binti wewe uko ugenini unaamka saa nne asubuhi, wenyeji wameshakwenda kazini unatoka chumbani na khanga moja unajaa siting room. Unasikia njaa huyo umesafisha meno na kutengeneza toast umerudi kutafuta cha kuangalia kwenye TV.

Wenyeji wana rudi jioni ndiyo unajikurupusha kwenda kuoga, wala huna wasiwasi kuwa baba mwenye nyumba ni jinsia ya kiume maungo inabidi uyastiri. Unapita na khanga moja kutoka bafuni.

Mwenyeji wako ni auntie ambae ameshakuwa na mashaka na ugeni huu. Akirudi na tiketi yako ya kurudi kwenu Tandahimba unaamni kuwa auntie ni mbaya hapendi kusaidia ndugu.
 
Halafu ukute binti mgeni ana chura kumzidi auntie yake, akijizungushia hiyo kanga moja, wanaume wenyewe hawa!!!

Ukiwa na mvuto katika familia hayo yategemee sio rahisi ndugu zako wa kike kukukaribisha kwao na huwa kunakakutengwa flani hivi japo na huyo binti hajafanya poa kuamka saa nne
 
Utashangaa mume ghafla hapitii tena pub akitoka kazini ni home faster faster. Tena anaanza kutoa na pesa ya shopping kwa binti.
 
Akirudi nyumban mfundishe. Mama yangu anakauli moja mtoto wa kike ukimlea Kama Jipu La tako litatumbuka sehemu mbaya litakutia aibu. Jipu la tako likamue likishaiva
Wazazi wengine wanaamini house girl ndiyo wa kutandika vitanda na kuosha vyombo mwanae ni wa kusoma, kwenda tuition na kuangalia cartoons
 
Mara nyingi ni hawa tunao wapeleka boarding kuanzia darasa la kwanza binti wa darasa la saba hujui kutandika kitanda
Hapana anaweza kuanzia boarding kuanzia la kwanza na bdo anatabia nzuri, ni malezi ya wazazi ndo yanatakiwa 7bu wazazi weng wakiona wana Dada wa kazi hawa waambiii watoto wao wawai kuamka na kumsaidia na kazi zngne za nyumban...... Kwaio ni jukumu la wa mama kuwafundisha watoto wakiwa wadogo kuwai kuamka na kusaidia kazi ndogo ndogo za nyumban
 
Ni kweli kabisa mkuu, ikiwezekana dada weekend apewe off watoto wafanye shughuli zote za ndani
 
Ni kweli kabisa kwanza watoto wanapenda kuoga kazi kama sehemu ya michezo na ukuaji. Akiwa anapenda kuiga kuosha vyombo mpe sahani na kikombe chake cha plastic aoshe toka mitatu
Wahenga walinena.

''Samaki mkunje angali mbichi"

Wazazi na walezi tuchukue hatua kunusuru hili janga japo Digital inavuruga kweli kweli lakini akiwa anaweza kuwajibika kwa kazi zingine za lazima ndani nyumbani inapendeza sana
 
Hakuna kitu kinanishinda kama madada wa siku hizi.Yan mtu anakuja kukutembelea lets say mpenzi halafu mkoba umejaa SEASONS.Akifika ni mwanzo wa kuangalia seasons tu.
Hawezi kuona kama pachafu asafishe au kuna nguo chafu afue yeye ni seasons na kuomba apewe chips.Akipanda kitandani zero kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…