Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Wakiume ni 'bin'mfano
Osama bin Laden
Hemed bin Jumaa
John bin Paulo etc

et al
 
Hapana mkuu hapa umetuburuza,waarabu wanatumia BINTI kwa mwanamke yeyote ambaye hajaolewa,msinielewa vibaya mimi nilifanya kazi na mama mmoja wa ki-Lebanon umri wake ulikuwa mkubwa wakuweza kuwa hata bibi lakini alikuwa ni binti,ni pia kulikuwa msichana ambaye pia alikuwa hajaolewa,walikuwa wakimchukulia kuwa ni binti...kwa lugha nyingine wanachukulia binti ni mwanamke bikira hivyo kutomuita binti mwanamke ambaye hajaolewa ni kama umemdharau
Kwahiyo huyo bibi alikua bikra? Mkuu umeanza kuchungulia vikongwe
 
Kwa uelewa wangu hilo neno bin ni kwa kiswahili fasaha ni wa. Unaweza kuniiita JUMA bin Abdalah manaye ni JUMA wa Abdalah. Mana ya neno bin ni wa .inaonyesha huyu anamilikiwa na nani.ni kama binadamu mana yake ni wa ADAMU kiuhalisia. Mana yake Sisi ni wa ADAMU.Bin ADAMU = wa ADAMU.

Kwa kimasai ndio unaposikia Daniel ole Njoolay.ole ni wa . ila sio jina halisi ni kuonyesha kuwa daniel ni Wa njoolay.Christopher ole sendekeka. Yaani huyo Christopher ni wa Sendeka. Hata MTU akikuuliza huyu mtoto ni Wa nani utamjibu ni wa CHACHA . bin ni kiarabu likimaanisha wa. Hiyo inatumika kwa jinsia zote. Mfano kwa lugha ya kikurya ole/bin inatamkwa o pekee.mfano. MARWA o Mwita. Mana yake MARWA wa Mwita. Kwa kiarabu tungetamka MARWA bin Mwita na kwa kimasai tungetamka MARWA ole MWITA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kwa ufafanuzi
 
Dah..... Mathematically....
Kama a WOMAN inaleta a MAN...
Basi BINTI nayo italeta BIN...
rahisi tu[emoji13] [emoji13]

Sent from my beretta ARX 160 using JamiiForums Mobile App
 
Mtoto wa kiume huitwa "bin"
Hii ni kweli kabisa, isipokuwa nje ya utamaduni wa pwani sijaisikia, labda hapo na pale kati ya Waislamu. Hata kamusi zangu kuanzia Sacleux (alikusanya msamiati miaka 100 iliyopita) hadi TUKI (=sasa TATAKI, Chuo Kikuu cha Dar) zinataja "bin".
Kamusi ya TUKI Swahili-English: "bin nm [a-/wa-] son of: Khamis bin Abdallah, Khamis the son of Abdallah. "
Kamusi ya Kiswahili Sanifu³: "bin nm (-) [a-/wa-] mwana wa kiume wa: Juma ~ Ali"
 
Mada tamu hii....
Anyway mtoto wa kiume anaitwa shabab.....wakike anaitwa bint....

Kwa mujibu wa lugha ya kiarabu.

Hakuna so called Aisha bint Mohamad kurejea jinsia ya kike.

Wenye lugha yao ya kiarabu karibu kunikosoa
 
Naomba kuondolewa ujinga, nimeulizwa na mtoto mdogo anayesoma darasa la tatu nimeshindwa kumjibu na kuishia kumpigia stori nyingine ili asahau swali lake, lakini kamekomaa kila muda kananikumbusha.....sijui nani amekatuma!! Msaada tafadhali...
Mtoto wa kiume anaitwa jembe
 
Back
Top Bottom