Mtoto wa kike wa miaka 9 kulala na babake

Mtoto wa kike wa miaka 9 kulala na babake

Ulikuwaje ukawa single parent wakat unaonekana smart san dada? Nadhan kwa huyo jamaa umekosea njia.

Anyway, weaning huwa ni kumuachisha mtoto ziwa toka kwa mama ake ili aanze kujitegemea kula mwenyewe, ila hili la baba kulala na mwanae wa kike wa miaka 9 limekaa kiaina sana. Nafikiri kuna something behind, jaribu kupeleleza ili upate jibu sahihi.
 
Mimi ni single mother wa mtoto wa kike wa miaka 10. Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na single father mwenye binti wa miaka 9.

Watoto wetu wanasoma shule moja madarasa tofauti. Tulikutana kwenye mkutano wa wazazi shuleni. Hali ya kuwa single parent ilituunganisha, tukajikuta tupo mapenzini. Tumekuwa msaada kwa kila mmoja wetu kwenye malezi.

Hatuishi pamoja officially ila tunatembeleana na sleepovers za mara kwa mara.

Tatizo ni huyu mtoto wangu kupitia mpenzi wangu, anapenda kulala na babake. Babake anasema ndio yuko hivyo kwani ameanza kumlea toka ana miezi 6 na hivyo kubidi kulala nae toka umri huo. Ameshindwa kum'wean'.

Akilala peke yake au na mwanangu hapati usingizi, inabidi aje chumbani kwetu tulale nae, either hadi asubuhi au tumhamishe kwa kumbeba akiwa ameshalala.

Naomba ushauri nifanye nini kumsaidia huyu mtoto aweze kujitegemea.

Natanguliza shukran wapendwa.
Unajua watoto wa kike wanahitaji sana ukaribu wa wazazi hasa mama ndio maana baba ukisafiri watoto wa kike huhamia kulala na mama. Tofauti na watoto wa kiume hata mama akiondoka hata siku moja hawahamiii kulala master bedroom.

Huyo mtoto kisaikolojia hayupo vizuri, amekosa ile lovw from her mother. Anahitaji upendo zaidi kuliko kumtoa kulala na baba ake.

Kama mama unahitaji kuonyesha upendo wa hali ya juu sana hata kama sio mwanao. Siku ukimfanyia vibaya atajisikia vibaya sana kwani anajua wewe sio mama ake.

Hata wewe kuanza kulala na baba ake hajisikii vizuri, anaona unamnyima haki yake ya kuwa karibu na baba ake. Baba ake ndio kila kitu , ndio faraja yake. Hivyo nakushauri uwe makini na chochote unacho kifanya kinacho badili mfumo wa maisha yake.

Kumtoa kwa nguvu ni kumwonea kwa sababu wewe ndio mgeni, njia rahisi ni kumpenda hadi atakapo elewa kuwa wewe ni mama ake anaye weza kukuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndomana wazungu huwafundisha watoto wao mapemaaa kutolala na wazazi

Wanalala kwenye CRIB wadogo. Sisi waafrica kijifanya tunawapenda saana tunalala nao mwisho toto bado dogo linajua wazazi wanafanya nini usiku.

Screenshot_2019-01-14-07-20-47.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto anasumbuliwa na upweke kwa kuto kua na mama. Cha msingi huyu mama afanye kazi yake vyema mtoto asikumbuke mama ake mzazi.. huyu mama ndio kavamia.
Aisee kama haina ushemeji basi pia haina undugu, anyway miaka 9 ni wazi kabisa mtoto anaelewa zuri na baya so aambiwe tu kuwa haipendezi mtoto wa kike kukumbatia kifua cha babake ndani ya shuka moja kwa umri huo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto anasumbuliwa na upweke kwa kuto kua na mama. Cha msingi huyu mama afanye kazi yake vyema mtoto asikumbuke mama ake mzazi.. huyu mama ndio kavamia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama nilivyodokeza awali, sio kwamba tunaishi pamoja officially bali tunatembeleana na husleep over kwetu au kwao. Hivyo kuhusu kuvamiwa, unadhani baba aendelee kuwa single au awe kwenye mahusiano ya vichochoroni kulinda hisia za mwana hadi lini? Kwa mtizamo wangu sioni hekima ya mtoto wetu huyu kuendelea kulala na babake. Na anamjua mamake na hana connection nae kiasi babake anashukuru hata kitendo cha mtoto kukubali kusleep over kwangu. Tunalichukulia hili jambo kwa umakini wa hali ya juu kuepuka kuumiza hisia za mtoto ndio maana numewashirikisha ndugu zangu wa JF kwa ushauri.
 
Ulikuwaje ukawa single parent wakat unaonekana smart san dada? Nadhan kwa huyo jamaa umekosea njia.

Anyway, weaning huwa ni kumuachisha mtoto ziwa toka kwa mama ake ili aanze kujitegemea kula mwenyewe, ila hili la baba kulala na mwanae wa kike wa miaka 9 limekaa kiaina sana. Nafikiri kuna something behind, jaribu kupeleleza ili upate jibu sahihi.

Things happen. Nitaendelea kupelekeza na pia kutafuta njia ya kumsaidia.
 
Mimi ni single mother wa mtoto wa kike wa miaka 10. Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na single father mwenye binti wa miaka 9.

Watoto wetu wanasoma shule moja madarasa tofauti. Tulikutana kwenye mkutano wa wazazi shuleni. Hali ya kuwa single parent ilituunganisha, tukajikuta tupo mapenzini. Tumekuwa msaada kwa kila mmoja wetu kwenye malezi.

Hatuishi pamoja officially ila tunatembeleana na sleepovers za mara kwa mara.

Tatizo ni huyu mtoto wangu kupitia mpenzi wangu, anapenda kulala na babake. Babake anasema ndio yuko hivyo kwani ameanza kumlea toka ana miezi 6 na hivyo kubidi kulala nae toka umri huo. Ameshindwa kum'wean'.

Akilala peke yake au na mwanangu hapati usingizi, inabidi aje chumbani kwetu tulale nae, either hadi asubuhi au tumhamishe kwa kumbeba akiwa ameshalala.

Naomba ushauri nifanye nini kumsaidia huyu mtoto aweze kujitegemea.

Natanguliza shukran wapendwa.
Ndo malezi hayo. Pambaneni naye taratibu atazoea. Mtoto wako amewezaje kutokukutegemea kwenye kulala? Ulishamzoesha kulala peke yake?
 
Ndo malezi hayo. Pambaneni naye taratibu atazoea. Mtoto wako amewezaje kutokukutegemea kwenye kulala? Ulishamzoesha kulala peke yake?

Nilimzoeza kulala peke yake, ingawa nilimwanzisha akiwa na miaka 6 hivi.
 
Back
Top Bottom