Mwenenu binnassib
Member
- Sep 19, 2021
- 8
- 7
Mama Janet alimuona Mwanakombo katika haliile watoto wote wa mtaani na Mama Janet alimtambua Mwanakombo kwa jina la Chidy kwa mara ya kwanza anaingia jijini alishuhudia mdada mmoja aliyekuwa akiitwa Subira alivyokuwa akibakwa mara kwa mara baada ya kutambulika ni binti.
Subira alikuwa mke wa getho la machokoraa kila aliyejiskia alimbaka kunawakati walimbaka kwa zamu.
Kwa wakati huo usingeweza kujua kirahisi Mwanakombo ni mwanamke kwa sababu ya uchakavu uliotokana na maisha na hakuwa amefika umri wa kupevuka.
Baada ya Mama Janet kuona Mwanakombo au Chidy anatokwa na mchozi akamsogelea “wewe mtoto unakutwa na nini Chidy mtoto wakiune unalialia hivi.” Mwanakombo aliinua sura yake na kumtazama Mama Janet machozi yakazidi kumtoka Mama Janet alikaa chini.
Mwanakombo akasema “mama nafikilia maisha haya mpaka lini jana nimelala kituon bila kosa la uhalifu wowote zaidi ya kukosa makazi kuna wakati natamani geto langu liwe jela” Mama Janet akaguna kidogo “mmmmh.
Mwanakombo akaendelea “serikal inatuchukia bila hata ya kutuuliza kwanini tupo mtaani na sisi tumezaliwa kwani sisi sio watoto wa taifa hili la Afrika? Nachefuliwa sana na hii kauli ya kila mtoto ni mtoto wa taifa hili mzazi baada ya kumzaa amepewa tu jukumu la kumlea hata ikitokea kamchinja mwanawe atafungwa mbano anapokuwa hayupo mwanawe hatunzwi? Mama Janet alijiinamia nakujisemea kumbe huyu anaakili sana”.
Mteja mmoja aliyekuwa anakula aliyasikia maneno haya ya Mwanakombo akainuka akaenda nyuma ya banda hili la mama ntilie akawasogelea akasema “Dunia ni uwanja wa vita pambana misemo na kanuni zao nimiongozo ndani ya makaratasi tu isikuumize kichwa magereza nimengi kuliko vituo vya watoto yatima kwasababu wanajua mfumo wao unazalisha wahalifu zaidi na hata ukibahatika kuomba msaada katika vituo vya malezi maswali na vielelezo nivingi kuliko utakapo pandishwa kizimbani kama mhalifu.
Wote wawili wakamtazama akaingiza mkono mfukoni akalipa chakula alichokula kisha akampatia elf tano Mwanakombo “shika hii japo najua haitamaliza matatizo yako itakufuta jasho la siku tu hilo ndio daraja letu na wao wanajua watakula nini toka sasa mpaka mwakani kana kwamba wana ahadi ya uhai wao na mola hatujui tutakula nini tutakapo amka asubuhi mola akutie nguvu” Mwanakombo aliipokea kwa haraka sana ile pesa nakusema “Asante sana umenitia nguvu”.
Hebu tulidhike na mkasa huu mfupi niliotanguliza kwenu kisha tutafakar hiki alichosema Mwanakombo baada ya kupewa pesa "Asante sana umenitia nguvu" ndio nguvu anayostahiki kupewa? Leo Askali watamkama kipigo ndio zawadi yake hakuna anayetaka kujua kwanini yupo pale kila mmoja kwa mapenzi yake atamuita mzurulaji.
Kulazwa sero kwakukosa makazi tena kwa masaa kadhaa sio utatuzi hata tuwapoze kwa lugha tamu vipi haitawafaa kitu kuandaliwe utaratibu wa kuwahifadh kuwasikiliza yale yanayomkuta tukabeba mzigo wake uliomuelemea haisaidii kupiga vita wakiitwa watoto wa mtaani na wapo mtaani kweli tuwaite watoto wanaishi katika mazingira magumu wakati tumewatafutia nyumba za kuwahifadhi.
Mfumo unaosaidia kuongeza wahalifu mtaani si mfumo wa maendeleo ya jamii bali wachache yani aliyeiba kodi za wananchi anadunda aliyefiwa na wazazi au kutengana akakosa elimu ndio aonekane kibaka wakati hakuandaliwa mfumo wa kumsaidia punguza watasema tutawasaidia wangapi? Na kwao hili litakuwa swali la msingi sana.
Kuto kuchukua maamuzi nikujenga msingi imara wa uzalishaji wahalifu na kuuwa vipaji na maono makubwa kama ya Mwanakombo.
kila mtoto ni mtoto wa taifa hili isiwe kauli ya kumpana kisheria mzazi juu ya mwanawe iwe kanuni ya kumsaidia mtoto pale mzazi anaposhindwa au kuto kuwepo.

Attachments
Upvote
0