Mtoto wa Kiume naye ni Binadamu kama wengine, acha kumkataza kulia anapokuwa na maumivu

Mtoto wa Kiume naye ni Binadamu kama wengine, acha kumkataza kulia anapokuwa na maumivu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mtoto wa kiume anakuwa na hisia kwa namna yeyote vile kama binaadamu wengine. Ni vile wewe mzazi unamsaidia mtoto wako kukua kwa namna ambayo utamsaidia na kumuongoza.

Mtoto wa kiume anastahili kuogopa na hata kulia. Mzazi acha kumkataza mtoto wako wa kiume kulia maana tuna tabia ya kuwaambia mtoto wa kiume halii.

Tabia hii inawafanya watoto wakuwe katika misingi ya kuamini watoto wa kiume hawatakiwi kulia wala kuumia, hivyo wakiwa watu wazima wanajikuta wanabeba mambo mengi katika mioyo yao & wanashindwa kuhimili maumivu yake. Pia inaweza kuwaathiri kupata hata magonjwa ya hofu.

Kulia ni moja ya njia ya kutoa sumu moyoni au mwilini na njia ya kupunguza uwezekano wa kupata huzuni katika mioyo yao.

#Malezi
 
Mwanaume anatakiwa kuwa tough kimwili na kimaamuzi. Ukimruhusu aanze kulia lia hawezi kuja kuwa tough kwenye maamuzi, atalia lia sana hadharani na kufanya achukuliwe poa. Kataza mtoto wa kiume kulia lia
 
Sometimes ya Dunia yakinishinda uwaga nalia sana au nikipoteza nimpendaye uwaga nalia pia siwezi kujizuia kulia
 
Jikaze .mtoto wa kiume wewe wanaume hawalii lii ovyo... mwisho wa kunukuu.
Mwisho wa siku vikiwazidi wanaona bora wajimalize tu
 
Huko ni kujaribu kubadilisha maumbile,mtoto wa kiume alie tu kaburi atachimba nani?Kaburini ataingia nani?Ni kweli mtoto wa kiume anapata uchungu ila anafunzwa kubeba maumivu toka jandoni sasa kama watoto wa kiume mnawatia ganzi watalia sana mpaka ndani ya madela yenu.Kumbuka mtoto wa kiume anategemea akili yake karibu kwa kila kitu akilia kila kitu kina haribika tofauti na wakike anaweza kulia kwa makelele ndani akitoka nje balimi zinapanda tu.Azimio ni mtoto wa kiume hakuna kulia lia.
 
Sometimes ya Dunia yakinishinda uwaga nalia sana au nikipoteza nimpendaye uwaga nalia pia siwezi kujizuia kulia
Aah kamanda! Mi huwa silii nakaa mwenyewe tu hata masaa 5 nafikiri, najipa matumaini nachora ramani kibao kichwani ya kupata suluhisho ya hiyo changamoto na naomba msaada wa kifikra pale itakapobidi.
 
Jikaze .mtoto wa kiume wewe wanaume hawalii lii ovyo... mwisho wa kunukuu.
Mwisho wa siku vikiwazidi wanaona bora wajimalize tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanaume anatakiwa kuwa tough kimwili na kimaamuzi. Ukimruhusu aanze kulia lia hawezi kuja kuwa tough kwenye maamuzi, atalia lia sana hadharani na kufanya achukuliwe poa. Kataza mtoto wa kiume kulia lia
Sio swala la kuwa yeye ni binadamu....yeye ni binadamu wa pekee...unapomuambia asilie unamuandaa kwa masahibu yajayo ambayo husababishwa na watoto wakike kulelewa kwa kuaminishwa kuwa wataolewa na mume ndio atawahudumia....mbona watoto wa kike huwa wanakatazwa kufanya michezo au kazi fulani wakiambiwa kuwa ni za kiume!
 
Mtoto wa kiume anakuwa na hisia kwa namna yeyote vile kama binaadamu wengine. Ni vile wewe mzazi unamsaidia mtoto wako kukua kwa namna ambayo utamsaidia na kumuongoza.

Mtoto wa kiume anastahili kuogopa na hata kulia. Mzazi acha kumkataza mtoto wako wa kiume kulia maana tuna tabia ya kuwaambia mtoto wa kiume halii.

Tabia hii inawafanya watoto wakuwe katika misingi ya kuamini watoto wa kiume hawatakiwi kulia wala kuumia, hivyo wakiwa watu wazima wanajikuta wanabeba mambo mengi katika mioyo yao & wanashindwa kuhimili maumivu yake. Pia inaweza kuwaathiri kupata hata magonjwa ya hofu.

Kulia ni moja ya njia ya kutoa sumu moyoni au mwilini na njia ya kupunguza uwezekano wa kupata huzuni katika mioyo yao.

#Malezi
Kuna ukweli ndani ya hili, especially katika kupunguza uchungu na hasira, LAKINI, narudia tena LAKINI, kwa life letu la kibongobongo bora mtoto wa kiume apigwe biti tu asilielie ovyo. And the reason is, maisha ya watu weusi yana changamoto sana hasa hasa kijana anapozidi kuwa mkubwa. Mfano, atatoswa na kadem kazur, atachapiwa, akimaliza balehe atakosa ajira, iko siku ataibiwa kila kitu, kuna siku atalala njaa, kuna kupoteza wapendwa wake, kuna kutukanwa hadharani, kusingiziwa n.k. maswaibu ya mwanaume ni mengi Miss Zomboko, so kijana akiona n sawa kulia lia trust me itabd atembee na bakuli la kubebea kamasi kwa maana atalia sana.
Yaan per day tu mwanaume anaeza akakutana na visanga kama 20 na vyote haviingiliani, bila moyo wa chuma hutoboi.
Hivyo basi, kama ni muhimu sana alie, mwambie inaruhusiwa kuwa na macho mekundu lakn sio kutwanga chozi kisoro!
 
Mwanaume haliii bali anainama na kusikilizia machungu baada ya hapo kazi iendelee..
 
Wakina mama nyinyi ndio mnatuharibia hawa kina "junior"

Hatupingi kulia anapoumia, lakini sio kulia lia hovyo, kujiliza liza, kuna namna mtoto wa kiume anapaswa kuwa, hiyo ni tofauti na mtoto wa kike. Mtoto wa kiume lazima aoneshe dalili za uanaume ndani yake, sio anaonesha dalili za "UMAMA"
 
Back
Top Bottom