Mtoto wa kiume unaweza kumwambia baba yako “I love you daddy” ?

Mtoto wa kiume unaweza kumwambia baba yako “I love you daddy” ?

Je ni baba yake mzazi au dadi kama dady maana humu mjini kuna watu ni wakuwaogopa hasa dady,anko,anti watu hawa ni hatari sana
 
Nilianza kumfundisha mwanangu wa miaka 9 Sasa Kila tukimaliza kuongea namwambia nampenda na yeye anasema ananipenda pia. Inaboresha mahusiano kati ya baba na mtoto. Mtoto anakua huru kuzungumza chochote
 
“Huyu jamaa yangu kanishangaza sana anamaliza call na mzee wake anamwambia “ i love you dady “ kuna vitu vingi vya kisasa kwa kweli mimi hapana “
Du!!!kazi kwelikweli ushawahi fika hata Dar wewe kweli?? hiyo Tecno unayotumia uliagiza???sasa kamwambie babayako I hate you baba!!!!
 
Hiyo haifai, hata katoto cha kiume kukabusubusu kama cha kike haifai
 
Sio tu i love you hata kuniita dady haifai, huu ndio mwanzo wa kuzoea kuita watu wazima dady na kuwaambia I love you, huu sio utamaduni wetu
 
Mzee wangu angenifukuza home au kuniitia kikao cha ukoo
 
“Huyu jamaa yangu kanishangaza sana anamaliza call na mzee wake anamwambia “ i love you dady “ kuna vitu vingi vya kisasa kwa kweli mimi hapana “
Tufanye alikuwa anaongea na mama yake, je angemaliza na kusema I love you Mama, ungeona ni sawa?
 
“Huyu jamaa yangu kanishangaza sana anamaliza call na mzee wake anamwambia “ i love you dady “ kuna vitu vingi vya kisasa kwa kweli mimi hapana “
Wewe na huyo jamaa yako wote ni wapuuzi tu.
 
Back
Top Bottom