Mtoto wa kuku anaumwa

Mtoto wa kuku anaumwa

no nm

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
212
Reaction score
32
Anayeufahamu huu ugonjwa pamoja na tiba tusaidiane. Uangalie kwenye picha hii Natanguliza shukrani.
 
Attachments

  • 09-04-15-14-47.jpg
    09-04-15-14-47.jpg
    5.6 KB · Views: 264
Kwanza mtenge na wenzake halafu waone madaktari wa mifugo haraka. Si kwamba kadonolewa na wenzake?
 
Shukrani.

Ni ndui ya kuku unatakiwa kuwachanja haraka nenda maduka ya mifugo wanauza chanjo! Sasa hivi mtenge na umpe dawa ambazo utashauriwa na madokta wa mifugo na vitamini kwa wingi hauna tiba ni kuwahi uwachanje basi.
 
Kesha chelewa huo ugonjwa ukisha ingia basi hata ukipewa antibiotics hautasaidia kitu na wauzaji watakupa coz ni biashara lakini watakufa wote
 
Kesha chelewa huo ugonjwa ukisha ingia basi hata ukipewa antibiotics hautasaidia kitu na wauzaji watakupa coz ni biashara lakini watakufa wote

Hapana haisambai sana. Na ambaye bado ajashikwa itafanya kazi i used to use it...!
 
Kitaalamu ni marufuku/haitakiwi kumpa chanjo mnyama baada ya kupata ugonjwa, kwa kufanya hivyo unakua unazidisha tatizo, tubadilike wafugaji jamani "CHANJO INA RATIBA YAKE" sio wameumwa ndio tunakumbuka chanjo. Kuhusu hao "waliobaki" niseme tu kwamba kama hao vifaranga walikua wanalala, kula na kushinda pamoja basi kuna hatari kubwa ya maambukizi kuwa yamesambaa (sio lazima wawe wote wanaonyesha dalili) japokua inawezekana pia kua wengine wakawa wazima. Cha kufanya watenge hao wagonjwa, tafuta msaada wa karibu (afisa mifugo wa karibu nawe) akija hapo atakupa msaada stahiki. (kuna vitu huwa tunaangalia ambavyo inakua ni vigumu kusema nikiwa mbali na kwa picha hiyo moja tu), hata kama hao vifaranga watakufa, lengo ni kuepusha dhahama kama hizi kesho na kesho kutwa. Asante.

"""Mbeya moyoni"""
 
Back
Top Bottom