Philemon, point yako nimeipata ni nzuri na inaeleweka BUT kumbuka huko ni uchagani huko na bongo mjini kwa hao wahindi etc Nimekaa ulaya miaka mingi sana sijaona mtoto wa miaka 13 kwenda kuwasaidia wazazi hizo kazi unazosema everyday.Ulaya wanavyothamini mtoto kuwa mtoto?? haiwezekani, tena nchi niliyokaa mimi wakikugundua unafanya hivyo unaweza funguliwa kesi na jamaa wa child protection.Jamaa wa child labour nao watakusakama hadi ukome ubishi....Anyway point yako naielewa, but tofautisha tu huko ni bongo na kule ni USA na hii dunia ya utandawazi mtoto anaweza akatengeneza pesa na akajifunza mengi sana mazuri at the same time akajifunza mengi machafu humu kwenye mitandao.Mwisho wa siku point yangu kuwa ilikuwa kusema Mange asipotoshe jamiii kuwa kwao wanazo sana wakati hali halisi inajieleza, aseme tu kuwa tunazitafuta kwa bidii zote na tunamshukuru mungu tunapatapata.Namna hiyo watu watajifunza na kupata moyo.Ila asubuhi kujifanya Oprah mchana unajifanya Bill Gates jioni unatangaza mtoto anauza pochi ili apate hela ya shule,wapi na wapi banaaa
Mbona ni kawaida sana kwa watoto wa ma celebrities kufanya either biashara au kufanya kazi. Will Smith ni actor mkubwa sana angalia watoto wake. Yule wa kiume, Jade akiw chini ya miaka 10 ameanza ku act. Alikuwa na ulazima gani kufanya kazi. Na yule wakike ameanza kuimba skiwa 13, anaingiza hela na wazazi wake pia wana hela.
Hapa wazazi waliangalia opportunity za watoto wao zitakazowasaidia ht wao wakiwa hawapo duniani.
David Beckham's family nao ni very rich na famous pia. Mtoto wao wa kwanza alianza kufanya kazi kwenye restaurant, na watu wengi walihoji, na wenyewe wakasema hata kama wazazi wana hela haimaanishi watoto wasifanye kazi kujitafutia future. Na watoto wao wengine wanashiriki u model.
Mifano ipo mingi sana ya watoto wa watu maarufu na wenye hela na wanafanya kazi na kuanzia miaka yoyote ile, ili mradi kuna opportunities kwao.
Ww unaeona cha ajabu Mange kumwanzishia biashara mwanae na unajinadi umekaa US hujaona kitu km hicho, itakuwa wazazi wao ni wauza sembe au viongozi mafisadi na nia yako Mange achukiwe ainekane kituko wakati ww ndio kituko.