KATASAN'KAZA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 3,097
- 1,356
Watu wenye akili nyingi sana za darasani mara nyingi maisha huwa yanawasumbua.
Dogo ana miaka hiyo,mkali wa namba!!
Mimi toka nikanyage secondary, marks nyingi kupata ni 21 kwenye mock form 2!!
Hesabu ni janga la kitaifa.
kubahatika kupata toto la hivi safi sana.... angekuwa Tanzania hakuna chuo ambacho kingemkubali
halafu ni mjaluo
Afu akili karithi kwa mamake...wale wanaobisha kuhusu hili wajionee wenyewe...
Kwani kuna anayebisha kwamba mtoto hawezi kurithi akili kutoka kwa mzazi wake?
Mtoto anaweza kurithi akili kutoka kwa mzazi yeyote yule, awe baba au mama.
Hivyo inawezekana kabisa karithi kutoka kwa mama yake na/ au inawezekana karithi kutoka kwa baba yake.
Au yawezekana kabisa karithi kutoka kwa babu au hata bibi.
Kuna mjadala naona wewe ulikupita...ngoja niishie hapa maana ubishi wake ulikuwa mkubwa...kwa wale walioshiriki wamenipata...
Hata mimi nna mdogo wangu ana umri wa miaka 6 tu anagonga CHEMISTRY NA BIOLOGY kinomaa!.lakini ndoivyo tu system ya kibongo hairuhusu, ingekuwa ulaya angeenda kusoma hata UDAKTARI
hahaaa!,......atii leta vyeti vya form 6.....lol!
Watu wenye akili nyingi sana za darasani mara nyingi maisha huwa yanawasumbua.
Vyuo vyetu viko sahihi.Mambo makubwa yanataka yaendane na umri mkubwa.Mtoto mdogo waweza hata mfundisha kuendesha gari,meli au ndege akaweza lakini huwezi mkabidhi mtoto wa miaka kumi kwa mfano aendeshe basi la abiria,meli au ndege ikiwa na abiria.Pamoja na kujua hajakomaa kufanya hizo kazi.Na kuna sheria za kuzuia mfano sheria ya ajira inakataza kuajiri watoto hata kama wana PHD ulimwenguni pote.
Hako katoto hata kakipata PHD huwezi kukaajiri sababu sheria za ajira duniani zinakataa ajira kwa watoto.
Akianza kujaza mambo makubwa mengi akiwa mtoto ubongo wake utachoka na kuchakaa haraka huko mbele hilo toto litakuwa boya.
Ndiyo maana mtoto inatakiwa aelimike taratibu kadiri akuavyo na akae na kukua na watu wa rika yake.Hebu fikiria mtoto wa miaka 10 yuko darasani na mijitu mizima darasani chuo kikuu inayoongelea kuachwa na boy friend au girl friend kimalezi unamwonea na kumchanganya sio mahali pake.Anatakiwa kuwa darasa lenye watoto wenzie wanaoendana.
Nakubaliana na wewe kabisa, ni bora mtoto afikishe umri na taratibu afuate mfumo uliopo. Mwanangu msichana alianza kwa fujo sana akiwa mdogo, tulimuona genious na nikaruhusu ajiunge na shule katika umri usiofaa, aliendelea kuwa namba moja darasani lakini baadaye akaanza kuboeka.
Sasa hivi yupo darasa la nane anasubiri kufanya mtihani wa KCPE lakini huwa tunahangaika kumsukumizia masomo. Kila akiamua huwa anafanya vizuri, ina maana bado mwereveu lakini kiaina tumeshindwa kumfanya azidi kupenda masomo.
Niliamua sitarudia hilo kosa, mdogo wake nilisubiri muda ufike na sasa huwa champion, kila muhula yeye namba moja na huwa amechangamka kweli. Ni bora mtoto aendane na wenzie katika umri.