Mtoto wa miaka 8 aliepotea Kibaha na kukutwa ametupwa shimoni na amekufa: Ni sahihi Polisi kusema usubiri masaa 24 kabla ya kuripoti kupotea mtoto?

Mtoto wa miaka 8 aliepotea Kibaha na kukutwa ametupwa shimoni na amekufa: Ni sahihi Polisi kusema usubiri masaa 24 kabla ya kuripoti kupotea mtoto?

polisi wa tz wanataka matokeo ya kesi kwanza sio kesi.unakumbuka yule marehemu aliyeshinda na polisi wiki zote wakati ndugu wakitafuta kijana wao.baada ya kuibuliwa na wakina malisa ndio wanajitokeza polisi kuleta mwili
 
Kiuhalisia polisi walipaswa kupokea report ya ya mtoto kupotea, though wasingejua pia wapi kwa kuanzia zaidi ya kuambatana na wazazi kutafuta maeneo anayopenda kwenda, kwa kesi kama hiyo ya mtoto kukutwa kwenye shimo la Choo ambacho hakijaanza kutumika unadhani polisi wetu wangetumia technology gani kujua alipo mtoto, zama hizi ni za kufunga watoto GPS tracker, mnunulie mtoto GPS watch n.k sababu hata case za watoto kuibiwa ni nyingi na huenda zika zidi kuelekea 2025 .
Watapokeaje taarifa wakati sheria ipo wazi kuwa mtu akipotea ili kufungua taarifa lazima yapite masaa 24?
 
Sheria karibia zote za Tanzania siyo nzuri na zina mapungufu makubwa kwa sababu mchakato mzima wa utungaji wa hizo Sheria umehodhiwa na kikundi kidogo Cha Watu wachache 'wenye muono mfupi kiakili (a short-sighted mind people).'
Njia pekee ya kuondokana na janga hili ni umma mpana wa wananchi kushirikishwa kikamilifu ktk michakato ya awali kabisa ya utungaji wa Sheria hizo, public participatory approach inatakiwa Sana ktk utungaji wa Sheria nchi.
Tatizo ni kwamba Watanzania huwa hatuna msukumo wa kutakakubadilisha mambo kwa pamoja. Kila tatizo linalotokea unaona kama wewe halikuhusu au halitatokea kwako. Mtu atasoma kwamba kuna mtoto wa miaka 8 aliripotiwa kupotea Polisi wakasema subiri masaa 24, unaona sawa tu, hadi siku ukipotelewa mtoto ndio utakapojua ubaya wa utaratibu kama huo
 
Hawa polisi wanachofatilia kesi yenye pesa km kukamata mwizi au mtu aliyekutukana.
Apumzike kwa amani mtoto pole kwa familia.
Hapo kibaha sijui km kuna usalama, hata kuna uzi uliwahi kuletwa mtu kauwawa na polisi wamekaa kimya hawafatilii
 
Kupokea tu taarifa mizengwe. Kweli kunaweza kuwa na utafutwaji wa aliyepotea?
 
fikiria kwamba amepotea, hujui alipo, hujui kama amekula au la, hujui kama analia kwa uoga hapo alipo au la, hujui kama ana maumivu, analia kukuita umsaidie, hujui kama kuna mtu anamtesa, anamuumiza, anamfanyia vitendo vibaya kama ubakaji au ulawiti, anamchapa fimbo au ngumi kumlazimisha. Damu zinamtiririka sehemu sehemu, na amevimba viungo kadhaa vya mwili.
Inaumiza sana
Mwenyezimungu atuepushe
 
Back
Top Bottom