JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tukio hilo jana Desemba 27 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya mtoto huyo kunyakuliwa na Fisi na kutokomea nae kuelekea msituni.
Baba wa mtoto huyo aitwaye Marco Nyangela amesema alisikia yowe kutoka kwa wanakijiji wakisema mtoto wake ameliwa na fisi ndipo wakaanza kumsaka mtoto huyo na kuishia kuona damu zikiwa zimetapakaa kuelekea kwenye msitu huo.
Hadi kufikia leo Desemba 28/2022 asubuh wamefanikiwa kuona nguo alizokuwa amevaa mtoto huyo, fuvu la kichwa na ubongo pamoja na meno mawili.
Germanus Masala ni mwenyekiti wa kijiji hicho na Amede Ssteness àmbae ni diwani wa kata ya Mwabomba wamesema wataendelea kushirikiana na wanakijiji kuwasaka fisi hao huku wakiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa nyakati za usiku.
Chanzo: EATV